Thursday, May 1, 2014

KISWAHILI KIDATO CHA PILI MUHTASARI.


KISWAHILI KIDATO CHA 1

Malengo ya kufundisha KiswahiIi katika Shule za Sekondari  
Mafunzo ya Kiswahili katika shule za Sekondari, yanakusudiwa kuwawezesha wanafunzi:
1. Kuturnia Kiswahili kwa ufasaha katika fani zote za maisha.
2. Kuhakiki kazi za fasihi ya Kiswahili.
3  Kujenga tabia ya udadisi katika masuala ya lugha ya Kiswahili
4  Kuelewa kuwa Kiswahili ni sehemu muhimu ya Utamaduni wa Tanzania.
 MALENGO YA KIDATO CHA PILI
Mwanafunzi aweze:
1.      Kueleza vipera vya tanzu za fasihi
2.      Kufahamu mbinu za kifani za kila kipera
3.      Kufafanua dhima za vipera vya fasihi simulizi
4.      Kutunga na  kuhakiki kazi za fasihi simulizi
5.      Kufafanua maana na dhima ya mofimu
6.      Kueleza maana na dhima ya uambishaji
7.      Kufafanua maana na dhima ya mnyumbuliko
8.      Kunyumbua maneno
9.      Kujibu maswali kutokana na habari aliyoisikiliza au kuisoma
10.  Kubainisha mawazo makuu kutokana na habari aliyoisikiliza au kuisoma
11.  Kufupisha habari  aliyoisikiliza au kuisoma
12.  Kusimulia hadithi na mada anuwai
13.  Kuandika insha, barua, simu na hotuba
14.  Kubainisha utumizi wa maneno
15.  Kueleza  dhima ya rejesta
16.  Kutambua na kusahihisha makosa ya utumizi wa lugha
 
1.      FASIHI
a.      Fasihi kwa jumla
b.      Fasihi simulizi
2.      SARUFI
a.      Mofimu
b.      Uambishaji
c.      Mnyumbuliko

No comments:

Post a Comment