Friday, October 3, 2014

TAKADINI Na Benson Hanson {MBS}----KIDATO CHA 3 NA 4



                                       UHAKIKI : RIWAYA

                                                         TAKADINI

MWANDISHI
: BENSON HANSON.
WACHAPISHAJI : METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS.


MANDHARI : RIWAYA   hii  imetumia  mandhari  ya   Vijijini  katika  nchi   ya   Zimbabwe  katika  karne  ya   19. Katika  masimulizi  haya  ya   riwaya    mandhari   yake   inaweza   kugusa   vijiji  vya  nchi  nyingi   za   KIAFRIKA  ambazo  zipo  katika   dunia   ya  tatu. {  nchi  zinazoendelea }.

 MWAKA:  2004.


 MAUDHUI

DHAMIRA KUU :


UKOMBOZI WA KIUTAMADUNI
--Ndoa.
--Mirathi.
--Uhai
--Maamuzi.
--Mgawanyo wa kazi.
--Mgawanyo wa mapato na umilikaji wa mali.
--Elimu.
--Utu.

DHAMIRA NDOGO NDOGO
---Mapenzi.
---Ndoa.
---Imani Potofu / Dhana potofu.
---Upendo.
---Ujasiri.
---Malezi ya watoto.
----Umoja na mshikamano
---Elimu.
---Nafasi ya mwanamke katika jamii na ujinsia

WAHUSIKA
TAKADINI
---Huyu ndiye mhusika   mkuu  wa   riwaya   hii.

---Ni  mtoto  wa   kwanza  wa  Sekai.
---Ni   mlemavu{ Zeruzeru } na  ana  tatizo  la   mguu.
---Kijana   wa   Kiume.
---Ni  mchapakazi  na   mtu  anayependa  kujifunza.
---Ni   mwenye   huruma.
----Ni  mtiifu.
---Ni   jasiri
---Ni    mwanamapinduzi..
---Ni  mhanga   wa  mila  na   desturi    mbaya   zinazobagua   walemavu.
----Anafaa  kuigwa   na   jamii.

SEKAI :
---Huyu  ni  mhusika  mkuu  msaidizi.
---Ni  mke  wa   kwanza  wa   MAKWATI.
---Ni  mwanamke  mchapakazi.
---Ni   mhanga  wa   mila   na  desturi  zilizopitwa  na    wakati.
---Ni    mwanamapinduzi.
---Ni  mama   mzazi   wa   TAKADINI.
---Ni  jasiri.
---Ni  mwenye   huruma.
---Ni   mwenye   busara.
----Ni  mvumilivu.
----Ni   mnyenyekevu
----Ni    mchapakazi.
----Ni   MPOLE.
---Ni   mama   mzazi    na   mlezi   mzuri   wa   familia.
---Ni   mama   mwenye  UPENDO.
---Ni    mpishi   mzuri   wa   chakula.
---Anafaa  kuigwa   na   jamii.

MAKWATI
----Ni   mume  wa   SEKAI.
---Ni   baba   mzazi  wa  TAKADINI.  
---Ni   mume  mwenye  wake   wannne,
---Ana   UPENDO   kwa  mkewe.
----Ni   mwoga.
---Ni    mkale.
Wake   wengine   wa   MZEE   MAKWATI   ni   DARAI ,  RUMBIDZAI ,


WAHUSIKA   WENGINE
CHIVERO , MTEMI  MASASA, SHINGAI , TENDAI ,   Nhamo , Maishingai , Pindai , Ambuya  Tungai , Ambupa  Shugu ,  Pedeisai ,  Mtemi  Zvedi ,  Tupfmaneyi ,  Chengatai,  Chido ,  Ambuya  Rekai ,  Mtemi  Chinjeyari.

No comments:

Post a Comment