UTANGULIZI
Kila mzazi angependelea mwanae afanikiwe katika masomo na kufaulu mitihani yake. Pia kila mwanafunzi anahitaji kufaulu katika mitihani yake. Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao.
Kufaulu mtihani ni muhimu kwa malengo ya mwanafunzi, kwani
anaposhinda mitihani humwezesha kuwa na mtazamo wa juu kielimu, kwa mfano kupata
cheti, diploma au digrii, kitu ambacho humfanya afae kwenye kazi. Wakati
mwingine inakuwa ni viguinu kwa baadhi ya wanafunzi kumudu masomo na mitihani
yao. Wakati huohuo wapo baadhi yao ambao wao kufaulu mitihani si tatizo.
Sasa mtu anaweza kujiuliza, kwa nini wanafunzi wengine washindwe
na wengine wafaulu vizuri katika masomo na mitihani yao? Mafanikio katika masomo
na kufaulu mitihani kunahitaji uwezo wa asili, kufanya kazi kwa bidii na kufuata
kanuni na mbinu za kusoma.
Wanafunzi wengine huona ugumu katika masomo na kufaulu mitihani,
si kwa sababu hawana akili, bali hawafuati mbinu na kanuni ftilani za kusoma na
kufaulu mitihani. Wengi wana uwezo mzuri, kama watajifunza mbinu hizi. Mbinu na
kanuni hizi zinaweza kutumiwa na wanafiinzi wa shule za msingi, sekondari, vyuo
na hata vyuo vikuu.
Kanuni na mbinu za Kusoma ni kama ifuatavyo:
JIJENGEE NIDHAMU BINAFSI YA HALI YA JUU YA KUJISOMEA KILA SIKU.
-----Weka lengo maalum
la kusoma kila siku na litimize.
-----Weka ratiba ya kila somo na
ifuate.
-----Tenga muda wa kutosha kwa kila
somo.
----- Jiwekee muda wa kutosha kila
siku kwa ajili ya kazi za utoaji taarifa za masomo na projekti.
-----Uwe na mahali maalumu pa
kusomea.
------Epuka kitu chochote
kinachoweza kukufanya usisome vizuri.
---- Jisomee katika muda unaodhani
unataa zaidi.
-----Uwe na muda wa kupumzika kila
unapochoka kusoma.
----- Usifanye mambo mengi kwa
wakati mmoja. Kwa mfano, mapenzi au anasa za kimwili wakati ungali mwanafunzi.
Hivyo ni vikwazo masomoni.
---- Tafuta mahali pasipo na kelele
za aina yoyote.
----- Epuka vishawishi vinavyoweza
kukufanya uairishe kujisomea.
------Fanya mazoezi ya mwili mara
kwa mara.
JIANDAE MUDA WOTE SOMA KILA WAKATI NI MUDA WA KUSOMA---USIPOTEZE MUDA.
-----Kabla hujaanza kujisomea,
hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo.
----- Hakikisha kuwa mahaii pa
kusomea pana mwanga wa kutosha.
----- Epuka kusoma ukiwa umejilaza
kitandani.
----- Unapokuwa na matatizo
kimasomo, mwone mwalimu, anayehusika.
------ Uwe na muda mwingi wa
kujisomea kila siku, usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile
maongezi.
------ Jiandae kwa mtihani kila
wakati, usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mtihani ndipo usome.
----- Epuka kusoma hadi usiku sana;
utaharibu afya yako.
------ Hudhuria shughuli zote za
shule nje ya darasani.
KUWA KING" ANG"ANIZI , PIGANA , KOMAA , PAMBANA, KUWA MBISHI---USIKATE TAMAA
----Jenga tabia ya uvumilivu na
kamwe usikate tamaa wakati ugumu unapoibuka masomoni.
---- Jenga tabia ya kupania kufaulu
katika masomo yako.
----- Amini kuwa utafaulu.
-----Epuka kuwaonea wivu na
kujilinganisha na wengine kimasomo, bali, jifunze tu siri za mafanikio yao.
-----Chunguza masomo yao ili ujue
udhaifti wako uko wapi.
WAKATI UNAPOKUWA SHULENI , CHUONI
----Fika darasani kwa wakati
unaotakiwa ili usikose maagizo.
----Usikose kipindi bila sababu
maalumu.
---Wakati mwalimu hajafika
darasani, pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.
----Usisome mambo mengi kwa wakati
mmoja.
---Soma kazi zako zote za
darasani kabla ya kuanza darasa.
---Usiwe mtu wa kukaa tu
darasani, uliza na jibu maswali yanapoulizwa.
---Uwe mwanafunzi mdadisi wa
mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia.
----Wasilisha kazi za darasani kwa
wakati wake.
----Baada ya kipindi, pitia yale
uliyojifunza.
----Epuka kukaa kimya na nyuma ya
darasa, bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.
---- Jenga uhusiano mzuri kwa
walimu wako na kwa wanafunzi wenzako. Ukiwa na amani moyoni, utasoma na kuelewa.
Jistahi na kuwapenda walimu wako. Ukimpenda mwalimu utalielewa vizuri somo lake.
JINSI YA KUJIFUNZA LUGHA YOYOTE YA KIGENI--Mfano :-Kiingereza , Kifaransa , Kichina , Kijerumani , n.k
-------Kama unajifunza lugha ya
kigeni, Fanya marudio, mazoezi mengi na soma vitabu vingi vya hadithi vya lugha
hiyo.-
------ Soma ukiwa na kamusi na tafuta
maana ya neno usilolijua.
----- Jizoeze kusikiliza na kuongea
ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
-----Sikiliza mihadhara na redio
ili ujifunze kwa wengine wanavyotamka maneno.
----- Jikumbushe maneno magumu kila
siku.
------ Kila nafasi unayoipata itumie
kwa kusoma.
------ Pambana na sarufi za lughaya
kigeni kikamilifu.
------ Jifunze lugha ya kigeni kwa
kuongea mara kwa mara.
------- Ni jambo la busara kuwa na
usiku mmoja wa kupunzika katikajuma ambayo si Jumapili au Jumamosi.
JIHUSISHE NA WENGINE UNAPOKUWA MWANAFUNZI( JIJENGEE TABIA NJEMA )
----- Ni muhimu kujihusisha na watu
wengine, jambo hili litakufariji kimawazo.
-----Ni vizuri pia kuwa na
mwanafunzi mwenzio wa kujadili naye.
EPUKA HAYA UKIWA MWANAFUNZI
-----Epuka marafiki wabaya wenye
nia ya kukupotosha.
-----Epuka pombe, uvutaji wa
sigara, bangi na madawa ya kulevya. Huharibu ubongo na kudhoofisha afya.
----Jijengee tabia njema ya
kujizuia katika tamaa za mwili.
------Kabla ya mtihani, soma kwa
bidii sana usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.
--------Usiku unaofuatiwa na siku ya
mtihani uwe na muda wa kutosha wa kulala. Usisome hadi usiku wa manane.
------ Soma kwa mpangilio kila siku
ili kujiandaa kikamilifu kwa mtihani.
--------Siku ya mtihani, usifikirie
kushindwa bali uwe na imani kuwa utashinda. Ondoa wasiwasi na mashaka.
------ Wahi kwenye chumba cha mtihani
kwani kuchelewa huleta hofu.
------ Chukua vifaa vyote muhimu
katika mtihani kama vile kalamu, penseli na rula.
----- Soma maagizo ya mtihani kwa
uangalifu sana, na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa kufanya kabla ya
kujibu swali lolote.
-----Kabla hujaanza kujibu maswali,
angalia maswali ambayo ni rahisi kwako kujibu..
-----Jibu maswali rahisi kwanza na
kwa haraka ili upate muda wa kutosha kujibu maswali
magumu.
----------------------------------------------------------------------------------
"USHINDI NI WAKO UNASTAHILI "
TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI. SEE YOU AT THE TOP
Ndimi
Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet
Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki
,
Mwl Japhet Masatu ni
Mwalimu Kitaaluma , Kocha wa Maisha na Mafanikio
, Mshauri , Mwalimu, Mjasiriamali , Public
Speaker
KWA MAELEKEZO ZAIDI TUWASILIANE KWA
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
Tuma MAONI , USHAURI , CHANGAMOTO KWA EMAIL :
studentsgotz.9@gmail.com
No comments:
Post a Comment