Wanafunzi na watahiniwa wanapopata swali katika mitihani wanajukumu kubwa la kulielewa kablaya kulijibu.
Endapo mtahiniwa atakuwa anajibu swali lolote bila kulielewa
matokeo yake ni hasara; atashindwa mitihani! Kushindwa si lengo la mtahiniwa
yeyote yule. Ili kukwepa hilo, mtahiniwa lazima awe makini.
Mara nyingi maswali yanayoulizwa kwa watahiniwa ni yale
yanayozingatia mkondo maalum. Mtahiniwa anaweza kuambiwa aanzishe, abainishe,
ajadili, aeleze, alinganishe, ajadili, aeleze, alinganishe, afafanue, aonyeshe,
atofautishe na kadhalika. Tunadokeza mbinu kadhaa ambazo ni za msingi katika
kujibu maswali ya mtihani.
· Maswali ya Kujadili
Kujadili ni kuhoji, kuuliza au kusaili. Suala la kujadili
linahusu pande mbili. Kwa nini jambo limetokea? Kwa kawaida hutolewa kauli
fulani ambayo mwanafunzi anatakiwa akubali au akatae; au yote kwa pamoja. Ni
muhimu kuelewa yafuatayo:
· Swali linataka nini hasa?
· Je, kuna mambo chanya?
· Je, kuna mambo hasi? Yepi ambayo yanatakiwa kutajwa?
· Maswali ya Kulinganisha
Kulinganisha kunahitaji mambo makuu mawili. Mambo haya ni
(a) Yale yanayoeleza kufanana kwa vipengele vilivyo katika vitu tofauti na
(b) Kutofautiana kwa mambo katika vitu hivyo viwili. Baada ya kulinganisha kama swali linavyotaka, hatua nyingine muhimu ni kuangalia ufanisi wa kazi zote/vitu vyote viwili.
Maswali yanatakiwa yajibiwe kwa kufuata mtindo wa insha. Kila
kipengele kinachojadiliwa kinatakiwa kihusishwe katika vitabu vyote
ambavyo vinahusishwa katika swali.
No comments:
Post a Comment