Kila mzazi angependelea
mwanae afanikiwe katika
masomo na kufaulu
mitihani yake. Pia
kila mwanafunzi anahitaji
KUFAULU katika mitihani
yake . Walimu nao hujisikia
vizuri wakati wanafunzi
wao wanapofanya vizuri
katika mitihani yao.
KUFAULU mtihani
ni muhimu kwa
malengo ya mwanafunzi , kwani anaposhinda
mitihani humwezesha kuwa
na mtazamo wa
juu kielimu , kwa
mfano KUPATA CHETI , DIPLOMA
AU DIGRII, kitu ambacho
humfanya afae kwenye
KAZI. Wakati mwingine inakuwa
ni vigumu kwa
baadhi ya WANAFUNZI
kumudu MASOMO na
mitihani yao. WAKATI HUO
HUO wapo baadhi
yao ambao wao
KUFAULU MITIHANI si
tatizo.
Sasa mtu
anaweza kujiuliza , kwa
nini WANAFUNZI wengine
WASHINDWE na wengine
WAFAULU vizuri katika
Masomo NA MITIHANI
yao ? MAFANIKIO katika
MASOMO na KUFAULU
MITIHANI kunahitaji UWEZO
WA ASILI , KUFANYA KAZI
KWA BIDII na
KUFUATA KANUNI NA
MBINU ZA KUSOMA.
Wanafunzi wengine
huona ugumu katika
MASOMO na KUFAULU
MITIHANI , si kwa
sababu hawana akili ,
bali hawafuati MBINU
na KANUNI fulani
za KUSOMA na
KUFAULU MITIHANI. WANAFUNZI
wengi wana uwezo
mzuri , kama watajifunza mbinu
hizi.
Mbinu na
kanuni hizi zinazweza
kutumiwa na wanafunzi
wa SHULE
ZA MSINGI , SEKONDARI ,
VYUO na hata
VYUO VIKUU.
KANUNI ZA KUSOMA
{1}. Weka LENGO maalumu
la KUSOMA kila siku
na litimize.
{2}. Jiandae kwa mtihani
kila wakati , usingoje mwalimu
atangaze kuwa ataleta
mtihani ndipo usome. SOMA
KILA SIKU.
{3}.Weka RATIBA ya
kila somo na
ifuate.
{4}.Tenga muda wa
kutosha kwa
kila somo.
{5}.Uwe na mahali
maalumu pa kusomea.
{6}.Epuka kitu chochote
kinachoweza kukufanya usisome
vizuri.
{7}.Tafuta mahali pasipo
na kelele za
aina yoyote.
{8}.Usifanye
mambo mengi kwa
wakati mmoja.Kwa mfano ,
MAPENZI au ANASA
ZA KIMWILI wakati
ungali mwanafunzi.Hivyo ni
vikwazo masomoni.
{9}.Jijengee
tabia njema ya
kujizuia katika tama
za mwili.
{10}. Fanya
MAZOEZI ya mwili mara
kwa mara.
{11}.Jiwekee
MUDA wa kutosha
kila siku kwa
ajili ya kazi
za utoaji taarifa
za MASOMO na
PROJEKTI.
{12}.Ni jambo la
busara kuwa na usiku
mmoja wa kumpumzika
katika juma ambayo
si Jumapili au
Jumamosi.
{13}.Ni muhimu kujihusisha
na watu wengine ,
jambo hili litakufariji
kimawazo.
WAKATI WA
KUJISOMEA
{14}. Kabla
hujaanza kujisomea , hakikisha
kuwa zana zote
muhimu kwa kusomea
zipo.
{15}.Epuka
vishawishi vinavyoewza kukufanya
uairishe KUJISOMEA.
{16}.Tafuta mahali pasipo
na kelele za
aina yoyote.
{17}.Hakikisha
kuwa mahali pa
kusomea pana mwanga
wa kutosha.
{18}.Usisome
mambo mengi kwa
wakati mmoja.
{19}.Epuka
kusoma hadi usiku
sana; utaharibu afya yako.
{20}.Jisomee
katika MUDA unodhani
unafaa zaidi.
{21}.Epuka
KUSOMA ukiwa umejilaza
kitandani.
{22}.Uwe na MUDA
wa KUPUMZIKA kila
unapochoka KUSOMA.
{23}.Uwe na muda
mwingi wa KUJISOMEA
kila siku , usipoteze
MUDA kwa mambo
yasiyo ya lazima
kama vile MAONGEZI.
UNAPOKUWA SHULENI /
CHUONI / DARASANI FANYA
YAFUATAYO
{24}. Fika
darasani kwa wakati
unaotakiwa ili usikose MAAGIZO.
{25}. Usikose kipindi bila
sababu maalumu.
{26}.Wakati
mwalimu hajafika darasani ,
pitia yale uliyojifunza
kipindi kilichopita.Soma kazi
zako zote za
darasani kabla ya
kuanza darasa.
{27}.Wakati Mwalimu
anafundisha darasani SIKILIZA
KWA MAKINI kile
anachofundisha na mwangalie
machoni mwalimu usiangalie pembeni .
{28}.Baada ya kipindi , pitia yale
uliyojifunza.
{29}.Chunguza
masomo yako ili ujue
udhaifu wako uko
wapi.
{30}.Jenga tabia ya
UVUMILIVU na kamwe
usikate tama wakati
ugumu unapoibuka masomoni.
{31}.Jenga tabia ya
kupania KUFAULU katika
MASOMO yako. AMINI KUWA
UTAFAULU.
{32}.Usiwe
MWANAFUNZI wa kukaa
tu darasani, ULIZA na
JIBU MASWALI yanapoulizwa.
{33}.Epuka kukaa kimya
na nyuma ya
darasa , bali shiriki
katika mazungumzo ya darasani
na wenzako.
{34}.Ni vizuri pia
kuwa na MWENZAKO
wa kujadili naye.
{35}.Uwe
MWANAFUNZI mdadisi wa
mambo kwa walimu
na hata kwa wanafunzi
wenzako pia.
{36}. Wasilisha
kazi za darasani
kwa wakati wake.
{37}.Unapokuwa na matatizo
kimasomo, mwone mwalimu , anayehusika.
{38}.Hudhuria
shughuli zote za
shule nje ya
darasani.
{39}. Jenga
uhusiano mzuri kwa
walimu wako na
kwa wanafunzi wenzako.Ukiwa na
AMANI moyoni , utasoma na
kuelewa. JISTAHI na
KUWAPENDA walimu wako. Ukimpenda mwalimu
utalielewa vzuri somo
lake.
{40}.Epuka
marafiki wabaya wenye
nia ya kukupotosha.
{41}. Epuka POMBE ,
UVUTAJI WA SIGARA , BANGI na
MADAWA YA KULEVYA.Huharibu ubongo
na kudhoofisha afya.
KABLA YA
MITIHANI FANYA HAYA
{42}.Kabla ya mtihani , SOMA KWA
BIDII SANA usingoje
mtihani umekaribia ndipo
usome.
{43}.SOMA kwa mpangilio
kila siku ili
KUJIANDAA kikamilifu kwa
MTIHANI.
{44}.USIKU unaofuatiwa na
siku ya mtihani
uwe na MUDA
WA KUTOSHA WA KULALA.
KULALA.Usisome hadi
usiku wa manane.
SIKU
YA MITIHANI FANYA
HAYA
{45}.Siku ya mtihani , usifikirie kushindwa
bali uwe na
IMANI kuwa utashinda.ONDOA WASIWASI
NA MASHAKA.
{46}.Wahi kwenye chumba
cha mtihani kwani
kuchelewa huleta HOFU.
{47}.Chukua vifaa vyote muhimu
katika mtihani kama
vile kalamu, penseli na
rula.
{48}.Soma MAAGIZO YA
MTIHANI kwa uangalifu
sana, na hakikisha
uko makii kwa
kile unchotakiwa kufanya
kabla ya kujibu
swali lolote
{49}. Kabla
hujaanza kujibu maswali , angalia maswali
ambayo ni rahisi kwako
kujibu.
{50}.JIBU maswali
rahisi kwanza na kwa
haraka ili upate
MUDA wa kutosha
kujibu maswali magumu.
Asante sana wanafunzi
wangu wa SHULE
ZA MSINGI, SEKONDARI, VYUO
na VYUO VIKUU
kwa kusoma makala
hii nzuri sana. Mwandishi
wa makala hii
ni MWL JAPHET
MASATU , anapatikana kwa
+ 255 716 924 136 ,
EMAIL, japhetmasatu@yahoo.com , DAR ES
SALAAM, TANZANIA, AFRIKA YA
MASHARIKI.
MUNGU AWABARIKI WOTE
No comments:
Post a Comment