SILABASI YA KISWAHILI YA KIDATO CHA 5
Mukhtasari huu umeandikwa kwa kuzingatia
matokeo ya tathmini ya muhtasari wa 1976 iliyofanywa na Taasisi ya
ukuzaji Mitaala mwaka 1988. Mapendekezo hayo yalitokana na upimaji wa
uwezo wa wanafunzi na maoni ya
waalimu na wakaguzi.
Mada za mukhtasari huu zimepangwa kulingana
na vidato. Inashauriwa mada hizi zifundishwe kwa njia ya kuchanganya na si kwa
kufuata mtiririko wa mada uliomo kwenye muhtasari huu. Kwa mfano, katika wiki
moja, mwalimu anaweza kufundisha vipengele
vya fasihi simulizi kwenye kipindi kimoja, vya sarufi kipindi kingine na vya
utungaji katika vipindi vingine.
Mwalimu
anashauriwa kuzingatia yafuatayo
- Pamoja na njia/mbinu za kufundishia zilizoandikwa humu, mwalimu abuni njia nyingine kulingana na uwezo na vionjo vya wanafunzi wake.
- Atengeneze na kutumia vifaa vya kufundishia kulingana na mahitaji ya wanafunzi wake.
- Ajielemishe kwa kusoma maandiko mbalimbali yanayochapishwa kila wakati.
- Awe mfano mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili fasaha.
- Orodha ya vitabu vya kufundishia Kiswahili itakuwa ikitolewa na Wizara ya Elimu kila baada ya muda maalum.
- Muhtasari huu unahitaji vipindi kumi na viwili kwa wiki.
Malengo ya
kufundisha kiswahili katika shule za Sekondari
Mafunzo ya Kiswahili katika shule za Sekondari yanakusudiwa
kuwawezesha wanafunzi
- Kutumia Kiswahili kwa ufasaha katika fani zote za maisha
- Kuhakiki kazi za fasihi ya Kiswahili
- Kujenga tabia ya udadisi katika masuala ya lugha ya Kiswahili
- Kuelewa kuwa Kiswahili ni sehemu muhimu ya Utamaduni wa Tanzania
Malengo ya Kidato cha Tano
Wanafunzi waweze:
- Kufafanua chimbuko la Kiswahili
- Kueleza ukuaji na ueneaji wa kiswahili
- Kufafanua nadharia ya fasihi
- Kujadili dhima ya udhamini wa kifasihi
- Kujadili nadharia ya uhakiki wa kifasihi
- Kufafanua tanzu za fasihi simulizi
- Kujadili mbinu za kifani katika fasihi simulizi
- Kujadili ukuaji wa fasihi simulizi
- Kujadili uhifadhi wa fasihi simulizi
- Kuhakiki fasihi simulizi
- Kutunga kazi za fasihi simulizi
- Kufafanua tanzu za fasihi andishi
- Kujadili mbinu za kifani katika fasihi andishi
- Kujadili ukuaji wa fasihi andishi
- Kuhakiki kasi za fasihi andishi
- Kutathmini mitazamo ya wanafasihi
- Kutunga kazi za fasihi andishi
- Kutambua kauli ya Kiswahili
- Kubainisha virai na vishazi
- Kueleza muundo wa ngeli
- Kuchanganua sentesi kwa njia ya mishale na maelezo
- Kujibu maswali ya ufahamu
- Kujadili mada anuwai
- Kutumia taratibu za uandishi
- Kutumia lafudhi ya Kiswahili
- Kuandika insha, simu, mialiko na barua
- Kutambua mitindo anuai katika kuzungumza na kuandika
- Kutambua mbinu za kifani katika kuzungumza na kuandika
- Kueleza dhima za mbinu za kifani
- Kutathmini matumizi ya semi na tamadhali
- Kutambua makosa ya kisarufi na kimantiki
- Kusahihisha makosa ya kisarufi na kimantiki
No comments:
Post a Comment