SILABASI YA KISWAHILI YA KIDATO CHA 6
Mukhtasari huu umeandikwa kwa kuzingatia
matokeo ya tathmini ya muhtasari wa 1976 iliyofanywa na Taasisi ya
ukuzaji Mitaala mwaka 1988. Mapendekezo hayo yalitokana na upimaji wa
uwezo wa wanafunzi na maoni ya
waalimu na wakaguzi.
Mada za mukhtasari huu zimepangwa kulingana
na vidato. Inashauriwa mada hizi zifundishwe kwa njia ya kuchanganya na si kwa
kufuata mtiririko wa mada uliomo kwenye muhtasari huu. Kwa mfano, katika wiki
moja, mwalimu anaweza kufundisha vipengele
vya fasihi simulizi kwenye kipindi kimoja, vya sarufi kipindi kingine na vya
utungaji katika vipindi vingine.
Mwalimu
anashauriwa kuzingatia yafuatayo
- Pamoja na njia/mbinu za kufundishia zilizoandikwa humu, mwalimu abuni njia nyingine kulingana na uwezo na vionjo vya wanafunzi wake.
- Atengeneze na kutumia vifaa vya kufundishia kulingana na mahitaji ya wanafunzi wake.
- Ajielemishe kwa kusoma maandiko mbalimbali yanayochapishwa kila wakati.
- Awe mfano mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili fasaha.
- Orodha ya vitabu vya kufundishia Kiswahili itakuwa ikitolewa na Wizara ya Elimu kila baada ya muda maalum.
- Muhtasari huu unahitaji vipindi kumi na viwili kwa wiki.
Malengo ya
kufundisha kiswahili katika shule za Sekondari
Mafunzo ya Kiswahili katika shule za Sekondari yanakusudiwa
kuwawezesha wanafunzi
- Kutumia Kiswahili kwa ufasaha katika fani zote za maisha
- Kuhakiki kazi za fasihi ya Kiswahili
- Kujenga tabia ya udadisi katika masuala ya lugha ya Kiswahili
- Kuelewa kuwa Kiswahili ni sehemu muhimu ya Utamaduni wa Tanzania
Malengo ya Kidato cha Sita
Wanafunzi waweze
- Kufafanua dhima ya vyombo vya habari katika kukuza na kueneza kiswahili
- Kueleza maana na matumizi ya pijini, lahaja na kreole
- Kueleza maana na matumizi ya lugha ya kwanza, ya pili, rasmi na ya taifa
- Kujadili mbinu za kifani katik afsihi simulizi
- Kujadili ukuaji wa fasihi simulizi
- Kujadili uhifadhi wa fasihi simulizi
- Kuhakiki kazi za fasihi simulizi
- Kutunga kazi za fasihi simulizi
- Kuhakiki kazi za fasihi andishi
- Kufafanua maana matumizi na mipaka ya uhuru wa mwandishi
- Kuhakiki misimamo ya waandishi
- Kufafanua aina za maneno
- Kufafanua matumizi ya ngeli
- Kuchanganua sentesi kwa njia za matawi, majedwali, maelezo na mishale.
- Kujibu mswali ya ufahamu
- Kubainisha mawazo makuu
- Kutathmini habari
- Kujenga hoja
- Kuandika insha, risala, hotuba, matangazo na barua
- Kutambua mitindo ya uzungumzaji na uandishi
- Kutumia sanaa ya uzungumzaji hadharani
- Kuhakiki fani katika fasihi
- Kutambua makosa ya kisarufi na kuyasahihisha
- Kujadili dhima ya rejesta katika lugha.
MADA
No comments:
Post a Comment