Saturday, September 7, 2019

SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU

Habari natangazia, Kuwapatia uhondo
Nchini Tanzania,   Kijiji cha  Loliondo
Watu viguu na njia, Wanoenda kwa vishindo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Siku imepambazuka, Naamshwa kwa kelele
Najifunga yangu shuka, Kutazama walo mbele
Tayari washazunguka, Kwa Kasisi Ambakile
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Miujiza imefika,  Babu yeye keshaota
Wote mloathirika, Anzeni kujikokota
Loliondo mkifika,  Mizizi inatokota
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Iwapo una nafasi,  Usiende mhimbili
Ondoa na wasiwasi, Loliondo kuna dili
Dawa bei ni rahisi, Kikombe ni buku mbili
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kashinda madakitari, Walosoma hadi ng’ambo
Magonjwa yote hatari, Yalokuwepo kitambo
Eti mpaka kisukari,  kweli babu ana mambo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Ukimwi unatutisha, Ugonjwa kama adhabu
Waganga wamechemsha, Kutafuta matibabu
Kama mbinu zimekwisha, Kajaribuni kwa babu
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kwa babu kuna vioja, Kabla kutoa tiba
Hutangaza yake hoja, Dawa msije kuiba
Mnapata mara moja, Sio kunywa mkashiba
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Wala msifanye pupa,  Walokwenda ni umati
Babu dawa akikupa,  Kunywa  kwa kombe la bati
Usipeleke na chupa, Ukayavunja  masharti
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Aponya kila madhara, Hili wengi wanakiri
Pengine ni  biashara, Katumia muhubiri
Kujitoa  ufukara,  Ajipe na utajiri
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Mara bibi wa tabora, keshaibuka na yake
Kujiona ndio bora, Na yeye afaidike
Watu kweli ni wakora, Jamani tuwajibike
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Sijui kama ya kweli, Msije mkasusia
Mi nahisi utapeli,  Mbuzi ndani ya gunia
Dawa sijaikubali,   Maajabu ya dunia?
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Namefika kaditama,  Dawa zinanitatiza
Babu ataniandama,  Malenga kuniapiza
Ninaogopa lawama,  Shairi nimemaliza
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
HAMZA A. MOHAMMED

Saturday, August 31, 2019

KISWAHILI---DARASA LA SABA ( STD 7 )---MASWALI YA KUJIPIMA-----TANZANIA----- ( PDF )

TRIAL EXAMINATIONS---STANDARD FOUR ( STD 4 )--( C ) ----MATHEMATICS, ENGLISH LANGUAGE , CIVIC AND MORAL EDUCATION , SCIENCE AND TECHNOLOGY, KISWAHILI , SOCIAL STUDIES----FOR ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOLS---TANZANIA------ ( PDF )

SWALI : Kwa Kutumia Mifano Eleza tofauti kati ya Fasihi Ya Kiswahili Na Fasihi Kwa Kiswahili ------FASIHI YA KISWAHILI NA FASIHI KWA KISWAHILI ------------------( PDF )

ELIMU YA DINI YA KIISLAMU 2---KIDATO CHA NNE ( F 4 )---CSEE, NECTA 2018----NOVEMBA-----TANZANIA-------- ( PDF )

ELIMU YA DINI YA KIISLAMU 1---KIDATO CHA NNE ( F 4 )---CSEE--NECTA 2018----NOVEMBA----TANZANIA------- ( PDF )

ARABIC LANGUAGE---FORM FOUR ( F 4 )---CSEE--NECTA 2018 -----NOVEMBER ------TANZANIA------ ( PDF )

AGRICULTURAL SCIENCE 2 ( PRACTICAL )----FORM FOUR ( F 4 )---CSEE--NECTA---2018----NOVEMBER---TANZANIA---------- ( PDF )

AGRICULTURAL SCIENCE 1----FORM FOUR ( F 4 )--CSEE ,NECTA , 2018 NOVEMBER----TANZANIA------ ( PDF )

Saturday, August 24, 2019

KISWAHILI--KIDATO CHA NNE ( F 4 )---MTIHANI WA UTAMILIFU--MOCK----AGOSTI , 2019----SHULE YA SEKONDARI SHAABAN ROBERT , DAR ES SALAAM --TANZANIA------ ( PDF )

MASHAIRI YA MNYAMPALA---DIWANI YA MNYAMPALA-----BY MATHIAS E. MNYAMPALA--------TANZANIA---------- ( PDF )

KISWAHILI---KIDATO CHA PILI ( F 2 )----MTIHANI WA UTAMILIFU / MOCK---2109---HALMASHAURI YA MJI KASULU --KIGOMA----TANZANIA------- ( WORD )

FORM TWO ( F 2 ) MOCK EXAMINATIONS----AUGUST , 2019---KISWAHILI , ENGLISH LANGUAGE , CIVICS , HISTORY , GEOGRAPHY , BIOLOGY , CHEMISTRY , PHYSICS , BASIC MATHEMATICS-----TAMONGSCO HIGHLANDS ZONE ACADEMIC COMMITTEE-----TANZANIA ------- ( PDF )

OSW 121 / 131 : UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU---FULL STUDY NOTES / MODULE---CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA-------- ( PDF )

Sunday, August 18, 2019

LUGHA NA UTAMADUNI---NADHARIA YA SAPIR ---WHORF

Mnamo karne ya 20 wanaisimu mahiri waitwao Edaward Sapir na Benjamin Whorf walitafiti lugha za Amerindia Amerika kaskazini na kugundua kuwa miundo ya msamiati na ya kisarufi ya lugha hizi haifanani kabisa na ile ya lugha ya kiingereza na lugha nyenginezo za Ulaya na Asia. Hivyo wakapendekeza nadharia isemayo kwamba  Lugha hutawala namna ya wazungumzaji wake waionavyo dunia. Ukichunguza baadhi ya misamiati ya wana lugha fulani utakuta kuwa yapo maneno pekee yanayowakilisha yale wayaonayo mbele ya macho yao au mazingira yao tu na kutokuwepo kwa neno kuna maanisha kwamba jambo hilo halipo ‘machoni’ pao. Sawa na kusema kuwa ‘lisilokuwepo machoni na moyoni halipo’. Nadharia hiyo ya Sapir- Wholf, inayojulikana kama nadharia ya Taathira lugha inaunga mkono mawazo ya awali ya Willian von Humbolt (1767-1835) pale aliposema kuwa ‘lugha ya mtu hutawala mawazo yake’. Si wote wanaokubaliana moja kwa moja na ule mtazamo kuwa lugha hufinyanga uoni wetu wa dunia, wao huchukulia kwamba lugha ‘huakisi’ utamaduni wa wazungumzaji wake. Mjadala huu unaendelea na wanafunzi wana fursa ya kuendelea nao na kuuchambua kwa kufatilia kazi mashuhuri ya hivi karibuni ya George Lakoff na Mark Johnson (1980) iitwayo Metaphors We Live By ambayo ina unga mkono mawazo kuwa lugha hutawala uoni wetu wa mazingira yanayotuzunguuka wanasema kuwa:
Dhana tulizonazo huunda kile tukionacho, kutuzunguuka na kinachotuhusu. Mfumo wa dhana ndiyo muhimili wa jinsi tuionavyo dunia yetu ya kila siku.
Nida ( 1986) anasema kuwa, lugha ni kielelezo cha utamaduni wa wazungumzaji wake na sio muhimili wa uoni wao. Lugha hufuata jamii na wala si kuingoza jamii hiyo (Nida, 1986:11)

Angalia:

  • Lugha ni sauti za nasibu zinazotumiwa na watu katika kuwasiliana miongoni mwao.
  • Jamimi ni kundi la watu wanaoishi pamoja na wenye kuhusiana kijamii, kikazi au kiuchumi na yenye kutumia lugha moja kwa ajili ya mawsiliano yao.
  •  Lugha imefungamana na jamii kiasi kwamba haiwezi kutenganishwa na maisha ya kijamii ya binadamu.
– Isitoshe lugha ni sehemu ya jamii kwani jamii haiwezi kuitumia na kisha kuiacha na kuchukua nyingine.
– Lugha ni kielelezo cha mahusiano ya kijamii yaani hueleza jinsi jamii inavyohusiana na mazingira yao halisi na namna wanajamii wanavyohusiana wenyewe kwa wenyewe.
– Lugha hubadilika  kulingana na mabadiliko ya kijamii. Pamoja na uhusiano huu baina ya jamii na lugha, hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya lugha na jamii kwa sababu:
i) Lugha sio lazima iwe ya watu wa jamii ile ile. Mathalani Kiswahili sio lugha ya Waswahili peke yao.
ii) Watu wanaoishi katika nchi sio lazima wawe wa asili ya nchi hiyo, kwa hivyo jina la jamii yao haiwezi kuwiana na lugha wanayoongea.
iii) Lugha moja huwa na vilugha kadha ndani mwake, mathalani lugha ya Kiingereza ina viingereza yaani lahaja kadha, mfano: Kiskochi, Kikoknii, Kilancastar n.k.
iv) Kuna jamii yenye jina tofauti na lugha wanayozungumza, mathalani Marekani hawazungumzi Kimarekani bali Kiingereza, Tanzania   kuna Kiswahili na sio Kitanzania

SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE

SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE
**********
Siwezi kukukumbuka,
kimya kimya mtukuka,
mwelekezi muafaka,
u wa maana hakika,
ut’endelea tajika,
milele yote milele.
****
Kwa dhati toka moyoni,
ni shahidi Maanani,
Baba ali mhisani,
wa wanyonge niamini,
alikuwa ni makini,
wa haki za binadamu.
****
Nyerere wetu shujaa,
Afrika aliifaa,
wasifa wake wajaa,
yote yote mataifaa,
mengi mema ulifanzaa,
nakuenzi Kambarage.
****
Shukurani Maanani,
kunigea tungo hini,
nikimtaja mwendani,
aliyeko mtimani,
kulla wa bora imani,
amkumbuke Nyerere.
***

Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.

USHAIRI---JINSI YA KUJIBU SWALI LA VITABU ( USHAIRI ) KIDATO CHA 5 & 6 ----------- ( PDF )

Thursday, July 11, 2019

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU---GATSCEE---NECTA--2019

BOFY  HAPA / CLICK  HERE: MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU GATSCCE 2019

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU---GATCE---NECTA 2019

BOFYA  HAPA /  CLICK  HERE : MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU GATCE-NECTA2019

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU---DTE -----NECTA 2109

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU DTE 2019

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU---DSEE---NECTA 2019 TANZANIA

BOFYA  HAPA / CLICK  HERE :MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU--DSEE--NECTA-- 2019  TANZANIA

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA ( ACSEE )--NECTA 2019

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU DSEE 2019

Wednesday, July 3, 2019

BIOLOGY---FORM ONE--TERMINAL EXAMINATION--2016---MWANZA---TANZANIA-----( PDF )

BASIC MATHEMATICS--FORM ONE---MID--TERM EXAMINATION--AUGUST 2017---MWANZA----TANZANIA----- ( PDF )

INFORMATION AND COMPUTER STUDIES ( ICS )--FORM ONE---MID--TERM EXAMINATIONS--MARCH 2016--EAST COAST ZONE---TANZANIA------( PDF )

CIVICS--FORM ONE---TERMINAL EXAMINATION---JUNE 2016---MWANZA------TANZANIA------ ( PDF )

KISWAHILI--KIDATO CHA KWANZA ( F 1 )--TERMINAL EXAMS( MUHULA 1 )---MEI 2015 ---HALMASHAURI YA MWANZA---TANZANIA-----( PDF )

Sunday, June 30, 2019

INTRODUCTION TO COMPUTER SCIENCE---AFRICAN VIRTUAL UNIVERSITY----OPEN EDUCATIONAL RESOURCES----- ( PDF )

ENTREPRENEURSHIP AND SMALL BUSINESS---STUDY / LESSON NOTES BY PAUL BURNS----- ( PDF )

OLG 221 : BUSINESS RSEARCH METHODS AND PHILOSOPHY----STUDY / LESSON NOTES---FOR THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA----- ( PDF )

OME 212 : BUSINESS ENVIRONMENT AND STRATEGIES ------- ( PDF )

OME 312 : ENTREPRENEURSHIP AND BUSINESS PLANNING-----STUDY / LESSON NOTES----FOR THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA----- ( PDF )