KABLA YA MTIHANI
{1}.Usiku unaofuatiwa na siku ya mtihani uwe na muda wa kutosha wa kulala. Usisome hadi usiku wa manane. LALA MAPEMA SAA 4 USIKU NA AMKA SAA 11 ALFAJIRI.Utakuwa umelala SAA 8 kiafya ni nzuri . KUMBUKUMBU YA MASOMO itakuwa vizuri / Active.{2}. Siku ya Mtihani, Usifikirie KUSHINDWA bali UWE na IMANI kuwa UTASHINDA. ONDOA Wasiwasi na Mashaka.WAZA KUFAULU SIYO KUFELI.
{3}.Wahi kwenye Chumba Cha Mtihani Kwani Kuchelewa huleta HOFU.
{4}. CHUKUA Vifaa vyote muhimu katika mtihani kama vile KALAMU, PENSELI, na RULA.
{5}.SOMA RATIBA YA MITIHANI angalia MASOMO yako na ZINGATIA MUDA, MUHIMU KULIKO VYOTE .
{6}.JIKUMBUSHE KILA WAKATI KUHUSU SHERIA ZA MITIHANI.
{&}.Kama una TATIZO LA KIAFYA hakikisha Msimamizi wako ANAFAHAMU. Mweleze Mapema.
{7}.JIFARIJI ,angalia huku na kule Kuna Wenzako pia kama wewe WANAFANYA MTIHANI PIA. Uwepo wa Wenzako utakufanya uweze KUJIAMINI.
{8}. ACHA KUTAFUTA FEKI YA MTIHANI UTAFELI VIBAYA SANA.
NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI
{6}.FANYA SALA FUPI kimoyomoyo Kumwomba MUNGU akuondoe HOFU/ FEAR COMPLEX NA MASHAKA. OMBEA WENZAKO PIA.JIAMINI NA UTASHINDA.
{7}.JAZA NAMBA YAKO YA MTIHANI na Maelezo Mengine MUHIMU katika Karatasi ya kujibia.
{8}.SOMA MAAGIZO/ MAELEKEZO YA MTIHANI Kwa Uangalifu sana na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa Kufanya kabla ya KUJIBU SWALI LOLOTE.
{9}.Kabla ya Kujibu Maswali ya Mtihani ANGALIA MTIHANI WOTE.
{10}.Kabla hujaanza kujibu MASWALI , ANGALIA MASWALI ambayo ni rahisi kwako kujibu.
{11}.JIBU MASWALI RAHISI KWANZA na kwa haraka ili upate MUDA wa kutosha KUJIBU Maswali Magumu.
{12}.Usijibu Swali bila kuelewa linataka nini ? JIBU utakalojibu litakuwa tofauti na swali.
{13}. Kama ni Swali la INSHA orodhesha dondoo utakazotumia kujibia swali husika.
{14}. USIPOTEZE MUDA KUNAKILI SWALI TENA. Andika Namba ya swali na jibu lake.
{15}.Usiwe na haraka ya Kumaliza mtihani kutakufanya Usijibu kwa makini.
{16}.KUWA NA SAA ya KUANGALIA MUDA Utakavyotumika wakati wa Kufanya Mitihani
{17}.Acha Nafasi kila baada ya SWALI kwa ajili ya Kuongeza nukuu zingine zitakazojitokeza baadaye wakati wa Kujibu Mtihani.
{18}. Kama MUDA umekwisha halafu bado unatakiwa kujibu Maswali Mawili au zaidi. JIBU KWA UFUPI kwa kila swali { OUTLINE ANSWERS }
{19}.Hakikisha unajibu swali sahihi bila kukosea namba ya swali. ANGALIA USICHANGANYE NAMBA YA SWALI. UTAKOSA MAKSI KWA KUJIBU SWALI AMBALO SIYO SAHIHI.
{20}. Tenga MUDA KIDOGO WA KUPITIA MTIHANI WAKO WOTE MASWALI PAMOJA NA MAJIBU YAKE.
{21}.Kila baada ya Kumaliza Mtihani USIPENDE KUJADILIANA MAJIBU YA MTIHANI WAKO PAMOJA NA MARAFIKI ZAKO. Itakufanya Ujenge HOFU na WASIWASI pindi utakapogundua umekosa swali. JIFUNZE KUSAHAU MTIHANI uliotoka Kufanya. ANGALIA Mitihani Inayokuja.
{22}.GAWA MUDA WAKO VIZURI.Angalia Idadi ya MASWALI Unayotakiwa Kujibu Na Jumla ya Muda wa Kumaliza Mtihani HUSIKA.
{23}. Hakikisha Unapanga Mtihani wako katika Mpangilio Mzuri Maswali na Majibu.
"MAY YOU BE SUCCESSFUL"
No comments:
Post a Comment