Tuesday, October 14, 2014

{1}.Msanii wa kazi ya Fasihi ni zao la jamii. Yote anayoyaandika katika kazi yake hutokana na jamii yake.Thibitisha ukweli au uongo wa kauli hii ukitumia vitabu viwili{2} kati ya TAKADINI , WATOTO WA MAMA N”TILIE na JOKA LA MDIMU




JIBU
          Msanii   wa   kazi  ya  Fasihi  ni  mtu  yeyote  anayejishughulisha  na  kazi  ya Fasihi  katika  jamii  yake. Hutumia   muda  wake  mwingi   kuzungumza  na  jamii  yake  kwa  njia   ya  maandishi. Huyu  ndiye  anayeelimisha , anayeburudisha , anayerithisha  utamaduni  wa  jamii  pamoja  na  kukuza  lugha  katika  jamii  husika.
            Nakubaliana  na   kauli  kwamba   msanii  wa   Fasihi  ni   zao   la   jamii  Fulani.  Yote  anayoyaandika  katika  kazi  yake  hutokana  na  jamii  yake.Hii  ni  kwa   sababu  fasihi   ni   zao   la   jamii  Fulani.Na   vile   vile  ndiyo  inayomzaa  na   kumlea   msanii.Nathibitisha  ukweli  wa   kauli  hii  kwa   kutumia  vitabu   vya    WATOTO  WA  MAMA   N”TILIE  na  TAKADINI.
           Katika  WATOTO   WA  MAMA  N”TILIE   mwandishi  amejadili   mambo  mbalimbali  yaliyomo   katika   jamii   zetu.Mambo  hayo  ni  kama  vile :
             ------Umaskini.
            ------Suala  la   Elimu.
             ------Suala   la   malezi.
             ------Ulevi.
             ------Nafasi   ya   mwanamke   katika  jamii.
            ------Mapenzi.
         Katika  TAKADINI  mwandishi  amejadili  mambo   mbalimbali  yanayojitokeza   katika  jamii   hususani  katika   nchi  zinazoendelea  ikiwemo   Tanzania. Baadhi   ya   mambo  hayo  ni :
              ------Mapenzi.
              ------Ndoa.
            -------Imani   potofu / Dhana   potofu.
            --------Upendo.
            -------Ujasiri.
            ------Umoja  na  mshikamano.
            -------Elimu.
            ------Nafasi   ya   mwanamke  katika   jamii  na  ujinsia.
            -----Malezi  ya  Watoto.
         Kwa   kuhitimisha, tunahitimisha    kuwa  Wasanii   wa   riwaya   za    TAKADINI , WATOTO  WA  N”TILIE   ni  zao   la  jamii  ya  Watanzania.Yale   yote    waliyoyaandika  katika  kazi  zao   yanatokana  na  jamii  ya  Watanzania.  Pia  jamii  ya  Watanzania   ndiyo   iliyowazaa  na  kuwalea  wasanii  hao.

No comments:

Post a Comment