Wednesday, March 25, 2020

MBINU NA KANUNI ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI

UTANGULIZI

Kila mzazi angependelea mwanae afanikiwe katika masomo na kufaulu mitihani yake. Pia kila mwanafunzi anahitaji kufaulu katika mitihani yake. Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao. 

Kufaulu mtihani ni muhimu kwa malengo ya mwanafunzi, kwani anaposhinda mitihani humwezesha kuwa na mtazamo wa juu kielimu, kwa mfano kupata cheti, diploma au digrii, kitu ambacho humfanya afae kwenye kazi. Wakati mwingine inakuwa ni viguinu kwa baadhi ya wanafunzi kumudu masomo na mitihani yao. Wakati huohuo wapo baadhi yao ambao wao kufaulu mitihani si tatizo.
Sasa mtu anaweza kujiuliza, kwa nini wanafunzi wengine washindwe na wengine wafaulu vizuri katika masomo na mitihani yao? Mafanikio katika masomo na kufaulu mitihani kunahitaji uwezo wa asili, kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni na mbinu za kusoma.

Wanafunzi wengine huona ugumu katika masomo na kufaulu mitihani, si kwa sababu hawana akili, bali hawafuati mbinu na kanuni ftilani za kusoma na kufaulu mitihani. Wengi wana uwezo mzuri, kama watajifunza mbinu hizi. Mbinu na kanuni hizi zinaweza kutumiwa na wanafiinzi wa shule za msingi, sekondari, vyuo na hata vyuo vikuu.
Kanuni na   mbinu  za Kusoma ni kama ifuatavyo: 

 JIJENGEE   NIDHAMU BINAFSI  YA  HALI  YA  JUU  YA  KUJISOMEA   KILA  SIKU.

 -----Weka lengo maalum la kusoma kila siku na litimize.
 -----Weka ratiba ya kila somo na ifuate.
-----Tenga muda wa kutosha kwa kila somo.
----- Jiwekee muda wa kutosha kila siku kwa ajili ya kazi za utoaji taarifa za masomo na projekti.

 -----Uwe na mahali maalumu pa kusomea.   
------Epuka kitu chochote kinachoweza kukufanya usisome vizuri.
 ---- Jisomee katika muda unaodhani unataa zaidi.
 -----Uwe na muda wa kupumzika kila unapochoka kusoma.
----- Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, mapenzi au anasa za kimwili wakati ungali mwanafunzi. Hivyo ni vikwazo masomoni.
---- Tafuta mahali pasipo na kelele za aina yoyote.
----- Epuka vishawishi vinavyoweza kukufanya uairishe kujisomea. 

------Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.



 JIANDAE  MUDA  WOTE SOMA  KILA   WAKATI  NI   MUDA   WA   KUSOMA---USIPOTEZE   MUDA. 
-----Kabla hujaanza kujisomea, hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo.
----- Hakikisha kuwa mahaii pa kusomea pana mwanga wa kutosha.

----- Epuka kusoma ukiwa umejilaza kitandani.
----- Unapokuwa na matatizo kimasomo, mwone mwalimu, anayehusika.
------ Uwe na muda mwingi wa kujisomea kila siku, usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile maongezi.
------ Jiandae kwa mtihani kila wakati, usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mtihani ndipo usome.
----- Epuka kusoma hadi usiku sana; utaharibu afya yako. 
------ Hudhuria shughuli zote za shule nje ya darasani. 
 
KUWA   KING" ANG"ANIZI , PIGANA , KOMAA , PAMBANA, KUWA   MBISHI---USIKATE   TAMAA   

----Jenga tabia ya uvumilivu na kamwe usikate tamaa wakati ugumu unapoibuka masomoni.
---- Jenga tabia ya kupania kufaulu katika masomo yako.
----- Amini kuwa utafaulu.
-----Epuka kuwaonea wivu na kujilinganisha na wengine kimasomo, bali, jifunze tu siri za mafanikio yao.
-----Chunguza masomo yao ili ujue udhaifti wako uko wapi.

     WAKATI  UNAPOKUWA  SHULENI  , CHUONI   
----Fika darasani kwa wakati unaotakiwa ili usikose maagizo.
----Usikose kipindi bila sababu maalumu.
 ---Wakati mwalimu hajafika darasani, pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.
----Usisome mambo mengi kwa wakati mmoja.
 ---Soma kazi zako zote za darasani kabla ya kuanza darasa.
 ---Usiwe mtu wa kukaa tu darasani, uliza na jibu maswali yanapoulizwa.
 ---Uwe mwanafunzi mdadisi wa mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia. 

----Wasilisha kazi za darasani kwa wakati wake.
----Baada ya kipindi, pitia yale uliyojifunza.

----Epuka kukaa kimya na nyuma ya darasa, bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.
---- Jenga uhusiano mzuri kwa walimu wako na kwa wanafunzi wenzako. Ukiwa na amani moyoni, utasoma na kuelewa. Jistahi na kuwapenda walimu wako. Ukimpenda mwalimu utalielewa vizuri somo lake.


JINSI  YA  KUJIFUNZA  LUGHA  YOYOTE  YA   KIGENI--Mfano :-Kiingereza , Kifaransa , Kichina , Kijerumani , n.k  
  
-------Kama unajifunza lugha ya kigeni, Fanya marudio, mazoezi mengi na soma vitabu vingi vya hadithi vya lugha hiyo.-
------ Soma ukiwa na kamusi na tafuta maana ya neno usilolijua.
----- Jizoeze kusikiliza na kuongea ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
-----Sikiliza mihadhara na redio ili ujifunze kwa wengine wanavyotamka maneno.
-----  Jikumbushe maneno magumu kila siku.
------ Kila nafasi unayoipata itumie kwa kusoma.
------ Pambana na sarufi za lughaya kigeni kikamilifu.
------ Jifunze lugha ya kigeni kwa kuongea mara kwa mara.
------- Ni jambo la busara kuwa na usiku mmoja wa kupunzika katikajuma ambayo si Jumapili au Jumamosi. 

JIHUSISHE    NA  WENGINE  UNAPOKUWA    MWANAFUNZI(  JIJENGEE  TABIA  NJEMA ) 
----- Ni muhimu kujihusisha na watu wengine, jambo hili litakufariji kimawazo.
-----Ni vizuri pia kuwa na mwanafunzi mwenzio wa kujadili naye.


EPUKA    HAYA  UKIWA   MWANAFUNZI    
-----Epuka marafiki wabaya wenye nia ya kukupotosha.
-----Epuka pombe, uvutaji wa sigara, bangi na madawa ya kulevya. Huharibu ubongo na kudhoofisha afya.
----Jijengee tabia njema ya kujizuia katika tamaa za mwili.

KABLA   YA   MITIHANI  FANYA   HAYA

 ------Kabla ya mtihani, soma kwa bidii sana usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.
--------Usiku unaofuatiwa na siku ya mtihani uwe na muda wa kutosha wa kulala. Usisome hadi usiku wa manane.
------  Soma kwa mpangilio kila siku ili kujiandaa kikamilifu kwa mtihani.
--------Siku ya mtihani, usifikirie kushindwa bali uwe na imani kuwa utashinda. Ondoa wasiwasi na mashaka.
------  Wahi kwenye chumba cha mtihani kwani kuchelewa huleta hofu.
------ Chukua vifaa vyote muhimu katika mtihani kama vile kalamu, penseli na rula. 

 UNAPOKUWA   NDANI   CHUMBA   CHA  MTIHANI  FANYA  HAYA
 ----- Soma maagizo ya mtihani kwa uangalifu sana, na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa kufanya kabla ya kujibu swali lolote. 
-----Kabla hujaanza kujibu maswali, angalia maswali ambayo ni rahisi kwako kujibu..
-----Jibu maswali rahisi kwanza na kwa haraka ili upate muda wa kutosha kujibu maswali magumu.
 ----------------------------------------------------------------------------------
           "USHINDI    NI    WAKO   UNASTAHILI "


TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.  SEE   YOU    AT   THE   TOP
 
Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 


Mwl   Japhet   Masatu  ni   Mwalimu  Kitaaluma , Kocha  wa Maisha  na   Mafanikio ,  Mshauri , Mwalimu,  Mjasiriamali , Public  Speaker


 KWA  MAELEKEZO    ZAIDI  TUWASILIANE   KWA



WhatsApp /  Call  / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539

Tuma   MAONI , USHAURI , CHANGAMOTO  KWA  EMAIL :
studentsgotz.9@gmail.com