Monday, September 9, 2019

UHAKIKI WA RIWAYA YA WASIFU WA SITI BINTI SAAD-----Na Shaaban Robert

KUHUSU SHAABAN ROBERT / ABOUT SHAABAN ROBERT

Shaaban Robert is to the Swahili language what Shakespeare was to English. Acclaimed as the national poet, his publications have always been the touchstone of beauty of language, purity of spirit, and deep wisdom informed by African and Swahili culture in particular, but imbued with respect for and understanding of other cultures. Most prominent of his work is Kusadikika (To be believed), an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. Published at the height of colonial occupation in Tanzania.

Shaaban Robert kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza. Akikubalika kama mshairi wa taifa, vitabu vyake daima vimekuwa kipimo cha juu cha uhondo wa lugha, usafi wa nia na hekima kutokana na utamaduni hususan wa Kiafrika na Waswahili lakini pia kwa jnsi alivyoelewa na kusheshimu tamadui nyingine. Katika vitabu vyake Kusadikika ndicho maarufu kushinda vyote. Hii ni hadithi ya kiistara juu ya nchi ambako dhuluma inatawala kinyume na haki, sheria na utu. Kitabu kilichapishwa wakati ukoloni umetanda nchini Tanzania.

WASIFU WA SITI BINTI SAAD-----RIWAYA / HADITHI-----BY SHAABAN ROBERT

Siti binti Saad alikuwa mwanamke wa kwanza Zanzibar kusimama jukwaani na kuimba nyimbo za taarab. Katika kitabu hiki, Shaaban Robert anaelezea juu ya maisha ya umaskini na hali ya chini aliyoishi msanii huyu, katika jamii ya Zanzibar iliyokitwa na tabaka za kijamii miaka ya kwanza ya karne ya ishirini. Licha ya kuwa sura yake ati haikuwa nzuri, alifikia hali ya juu ya nyota wa uimbaji wa taarabu akapendwa na wapenda taarabu si Zanzibar tu na Afrika ya Mashariki, lakini pia alipendwa hadi Misri na India. Kwa wapenzi wa taarab bado ni malkia, sawa na alivyokuwa Om Kulthum wa Misri. 
 Siti binti Saad was the first woman Taarab singer in Zanzibar. In this book Shaaban Robert looks at the background of the singer: poverty and low birth, in a society riven by class and race in early 20th century Zanzibar. Despite her so-called bad looks, she became a star whose voice was recognised and loved by many, not only in Zanzibar and East Africa, but as far as Egypt and India. She was and remains to taarab lovers, the equivalent of Egypt’s Om Kulthoum.

Sunday, September 8, 2019

ENGLISH LANGUAGE---STANDARD SEVEN ( STD 7 )---MOCK EXAMINATION----DAR ES SALAAM---TANZANIA-------- ( PDF )

SAYANSI---DARASA LA SABA ( STD 7 )---2019----MTIHANI WA UTAMILIFU---MOCK----MKOA WA DAR ES SALAAM----TANZANIA--------------- ( PDF )

MAARIFA YA JAMII---DARASA LA SABA ( STD 7 )--2019---MTIHANI WA UTAMILIFU / MOCK-----MKOA WA DAR ES SALAAM----TANZANIA--------- ( PDF )

FORMAT---DIPLOMA IN SECONDARY EDUCATION IN SPECIAL NEEDS EDUCATION ( DSE---SNE ) EXAMINATION FORMATS------ISSUED BY NECTA , AUGUST , 2012 --------- ( PDF )

FORMAT---DIPLOMA IN SECONDARY EDUCATION EXAMINATION FORMATS ( DSEE )----ISSUED BY NECTA , SEPTEMBER , 2010 ---------TANZANIA----- ( PDF )

FOMATI ZA MITIHANI YA UALIMU KWA NGAZI YA CHETI ( DARAJA LA A )---GATCE---GRADE A TEACHERS CERTIFICATE EXAMINATION FORMATS----IMETOLEWA NA NECTA, SEPTEMBA 2010--------- ( PDF )

NEW FORMAT---FORM TWO ( F 2 ) NATIONAL ASSESSMENT FORMATS ( FTNA )ISSUED BY NECTA , JANUARY , 2017--------TANZANIA-------------- ( PDF )

NEW FORMAT FORM FOUR ( F 4 )---CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION FORMATS---REVISED BY NECTA, FEBRUARY , 2019 -----TANZANIA------ ( PDF )

THE FORMAT FOR STANDARD FOUR ( STD 4 ) NATIONAL ASSESSMENT ( SFNA )---ISSUED BY NECTA , 2018 -----FOR ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOLS-----TANZANIA-------- ( PDF )

FOMATI MPYA YA UPIMAJI WA MTIHANI WA KITAIFA DARASA LA NNE-( STD 4---SFNA )--IMETOLEWA NA NECTA , FEBRUARI , 2018 -------TANZANIA------ ( PDF)

FOMATI MPYA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI----NEW PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION ( PSLE ) FORMAT----IMEREKEBISHWA , FEBRUARI , 2018 -------TANZANIA--------- ( PDF )

Saturday, September 7, 2019

SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU

Habari natangazia, Kuwapatia uhondo
Nchini Tanzania,   Kijiji cha  Loliondo
Watu viguu na njia, Wanoenda kwa vishindo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Siku imepambazuka, Naamshwa kwa kelele
Najifunga yangu shuka, Kutazama walo mbele
Tayari washazunguka, Kwa Kasisi Ambakile
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Miujiza imefika,  Babu yeye keshaota
Wote mloathirika, Anzeni kujikokota
Loliondo mkifika,  Mizizi inatokota
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Iwapo una nafasi,  Usiende mhimbili
Ondoa na wasiwasi, Loliondo kuna dili
Dawa bei ni rahisi, Kikombe ni buku mbili
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kashinda madakitari, Walosoma hadi ng’ambo
Magonjwa yote hatari, Yalokuwepo kitambo
Eti mpaka kisukari,  kweli babu ana mambo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Ukimwi unatutisha, Ugonjwa kama adhabu
Waganga wamechemsha, Kutafuta matibabu
Kama mbinu zimekwisha, Kajaribuni kwa babu
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kwa babu kuna vioja, Kabla kutoa tiba
Hutangaza yake hoja, Dawa msije kuiba
Mnapata mara moja, Sio kunywa mkashiba
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Wala msifanye pupa,  Walokwenda ni umati
Babu dawa akikupa,  Kunywa  kwa kombe la bati
Usipeleke na chupa, Ukayavunja  masharti
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Aponya kila madhara, Hili wengi wanakiri
Pengine ni  biashara, Katumia muhubiri
Kujitoa  ufukara,  Ajipe na utajiri
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Mara bibi wa tabora, keshaibuka na yake
Kujiona ndio bora, Na yeye afaidike
Watu kweli ni wakora, Jamani tuwajibike
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Sijui kama ya kweli, Msije mkasusia
Mi nahisi utapeli,  Mbuzi ndani ya gunia
Dawa sijaikubali,   Maajabu ya dunia?
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Namefika kaditama,  Dawa zinanitatiza
Babu ataniandama,  Malenga kuniapiza
Ninaogopa lawama,  Shairi nimemaliza
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
HAMZA A. MOHAMMED