TAFSIRI NA UKALIMANI
Tafsiri [Translation]
Dhana ya Tafsiri.
Tafsiri
imefasiliwa kuwa, ni Kutoa mawazo kutoka katika lugha moja kwenda lugha
nyingine bila ya kubadilisha maana. [TUKI 2002: 271]
Catford
[1965:20] anasema tafsiri ni, “Kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi
kutoka lugha moja {lugha chanzi} na kuweka badala yake mawazo
yanayolingana katika lugha nyingine {lugha lengwa}.
Vilevile imefasiliwa kuwa ni “Mawazo yaliyotolewa kutoka lugha moja hadi lugha nyingine.”
TUKI [2002: 271] Tafsiri ni kueleza maana ya maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.
Maana zote hizo tulizoziangalia, utaona kuwa, kuna mambo matatu muhimu yanayojitokeza, mambo hayo ni:
(i) Mawazo yanayotakiwa kutafsiriwa sharti yawe katika maandishi.
(ii) Mawazo au ujumbe kati ya lugha chanzi na lugha lengwa sharti yalingane.
(iii) Tafsiri inaweza kuwa kutoa maana ya maneno au mawazo.
Baada ya kuangalia maana ya tafsiri, sasa tuangalie maana ya mfasiri na sifa anazotakiwa kuwa nazo mfasiri:
Mfasiri
Mfasiri ni mtu anayefanya tafsiri kutoka lugha moja hadi lugha nyinge.[TUKI:2000:165]
Kwa
ujumla tunaweza kusema kuwa, mfasiri ni mtu anayehamisha mawazo kutoka
lugha moja (lugha chanzi) kwa kutumia lugha nyingine ili mawazo hayo
yaeleweke na watu wasiojua au kuielewa lugha chanzi, na mawazo hayo
sharti yawe katika maandishi.
Sifa za mfasiri bora
Mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
? Awe na ujuzi wa lugha fasaha, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani lugha chanzi na lugha lengwa.
?
Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini
chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha
katika lugha lengwa.
? Awe amesoma maandishi ya matini chanzi hadi ayafahamu kinaga ubaga halafu aweze kuyafikiria katika lugha lengwa.
Historia ya Tafsiri nchini Tanzania / Afrika mashariki
Taaluma
hii ya tafsiri ina historia ndefu hapa dunia tangu kale, lakini kwa
hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla historia hii ya tafsiri
haina historia ndefu kwani inaanzia karne ya 19 ambapo wamisionari
walitafsiri vitabu mbalimbali vya kikristo ikiwemo biblia kutoka lugha
ya kiingereza kwenda Kiswahili na lugha nyingine za makabila makubwa
nchini Tanzania.
Na hata wakati wa utawala wa kikoloni
hasa waingereza walitafsiri maandiko mbalimbali ya taaluma na fasihi ya
Ulaya kwa lugha ya Kiswahili Na hata baada ya uhuru wapo wazalendo
waliofanya juhudi za kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili
mfano mzuri ni Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere
ambaye alitafsiri vitabu viwili vya mwandishi mashuhuri wa tamthiliya wa
Uingereza William Shakespeare ambavyo ni: Juliasi Kaizari [1963] na
Mabepari wa Venisi[1969] {Tazama pia Mwansoko na wenzake 2006 : 5}
Mfano
wa tafsiri ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ni pamoja na
ya,Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa ambayo imetafsiriwa na Abdilatif
Abdalla, House boy ya Ferdinand Oyono iliyotafsiriwa na Raphael Khasao
na Nathan Mwele. Juliasi Kaizari na Mabepari wa Venisiza zaWilliam
Shakespeare zilizotafsiriwa na Julius K. Nyerere, Hekaya za Abunuwasi,
Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa, Alfu
Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton na Mashimo ya Mfalme
Suleiman kilichotafsiriwa na Sir Rider Haggard, Takadini,kimetafsiriwa
na Mathews Bookstore and Stationers, Nitaolewa Nikipenda ambacho
kimetafsiriwa na Crement M. Kabugi. vitabu vingine vilivyotafsiriwa ni
kama vile; Orodha, Barua Ndefu Kama Hii n.k.
Mpaka sasa wataalamu
mbalimbali wamekuwa wakiendelea kutafsiri maandiko mbalimbali kama vile
mikataba na ripoti mbalimbali za kimataifa, sheria ambazo mwanzo
zilikuwa zikiandikwa kwa lugha ya kiingereza, vitabu vya kiada na ziada,
kazi za kifasihi, n.k
Mambo ya kuzingatia katika tafsiri
Katika
sehemu hii tutaangalia mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa katika
tafsiri, hivyo basi, tutagawa mambo hayo ya kuzingatia katika sehemu
mbili, sehemu ya kwanza ni mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza mchakato
wa kutafsiri na sehemu ya pili, tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia
wakati wa mchakato wa kutafsiri. Tukianza na:
[a] Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza mchakato wa kutafsiri.
? Kwanza unatakiwa kusoma matini nzima.
Mtu
anayetaka kutafsiri matini yoyote ile jambo la msingi la kuzingatia ni
kuisoma matini nzima tena kwa umakini ili kuelewa maudhui ya matini
chanzi, kuweka alama sehemu za matini zenye utata au zisizoeleweka
vizuri, hii itamsaidia kubaini ni aina gani ya marejeo muhimu
yatakayomsaidia kutafsiri mfano wa marejeo hayo ni kama kamusi,
ensiklopedia, orodha ya msamiati na istilahi mpya.
? Unatakiwa kubaini lengo la matini chanzi
Baada
ya kuisoma matini chanzi, je! Umeweza kubaini lengo la matini chanzi ni
nini? Kubaini lengo la matini kutakusaidia kuweza kutafsiri bila
kutofautiana/kukinzana na lengo la matini chanzi, mathalani, matini
mbili tofauti zinaweza kueleza jambo lilelile na kutumia data zilezile
lakini mtindo wa lugha uliotumika unaweza ukaonesha mitazamo miwili
tofauti.
Hebu angalia tamthilia ya Mercant of Venice,
iliyoandikwa na William Shakespeare na kutafsiriwa na Mwalimu J.K.
Nyerere kwa lugha ya Kiswahili na kuitwa Mabepari wa Venisi, kumbuka
kuwa tamthiliya hiyo ingeweza kuitwa pia Wafanyabiashara wa Venisi
lakini ukiangalia tafsiri ya kwanza [Ya Mwalimu Nyerere] inatupa hisia
hasi wakati ya pili huwezi kupata hisia yoyote.{Mwansoko na wenzake
2006:15}
? Unatakiwa kubaini hadhira/ wasomaji lengwa.
Kabla
ya mfasiri hajabaini wasomaji au hadhira ya wasomaji wa matini yake ya
tafsiri ni vema kwanza akaibaini hadhira ya matini chanzi na ndipo
abaini hadhira/ wasomaji mahususi wa matini yake ya tafsiri, maswali
anayotakiwa kujiuliza mfasiri ili aweze kuibaini hadhira ya matini yake
ya tafsiri ni: je msomaji wa tafsiri yake ni nani? Ana kiwango gani cha
elimu, ni msomi wa kawaida au msomi aliyebobea? Wana umri gani na ni
jinsia gani? Je hadhira yake imo katika tabaka gani katika jamii? Baada
ya kupata majibu ya maswali hayo, mfasiri atakuwa ameibaini hadhira
yake,na hii itamsaidia mfasiri kuamua umbo la matini yake, kama ataamua
iwe katika umbo la gazeti, jarida, kijarida, n.k. jambo la kuzingatia
umbo la matini ya tafsiri ishabihiane na hadhi ya umbo la matini chanzi.
Kwa kuibaini hadhira ya matini lengwa itamsaidia mfasiri kuamua
kuirahisisha tafsiri yake au kuifanya iwe ngumu kutegemeana na uwezo wa
hadhira ya tafsiri lengwa.
? Unatakiwa kubaini mtindo wa matini chanzi.
Vilevile,
mfasiri anatakiwa kujua, matini chanzi imetumia mtindo gani katika
kuwasilisha maudhui yake, imetumia mtindo wa kirasimu? Au imetumia
mtindo wa kitaaluma? Je imetumia mtindo wa kiuandishi wa habari au
mtindo wa kimawasiliano yasiyo rasmi? Je ametumia lugha rasmi au ya
mtaani? Na inatakiwa mtindo wa matini chanzi ilingane na ile ya matini
lengwa. Tazama mifano ifuatayo:
Kingereza: Please, Sir do no mind it! If I arrive earlier I’ll wait for you
Kiswahili: Mkubwa! Kausha tu! Na kama nitatia maguu mapema,
nitakusikilizia Palepale
Ukiangalia
mfano huo, utaona kuwa, mitindo iliyotumika katika sentensi hizo ni
mitindo miwili tofauti, katika mfano tuliouangalia katika lugha chanzi,
mtindo wa lugha uliotumika ni mtindo rasmi, wakati katika tafsiri [lugha
lengwa] mtindo uliotumika ni mtindo wa lugha ya mtaani, jambo ambalo si
zuri katika tafsiri. Mtindo wa lugha lengwa sharti ulingane na mtindo
wa lugha chanzi.
hivyo katika mfano huo, mtindo sahihi ungetakiwa kuwa;
Tafadhari! usijali! kama nitafika mapema, nitakusubiri.
? Kusoma matini kwa mara ya mwisho
Jambo
lingine la kuzingatia ni kuisoma upya matini chanzi. Katika kipengele
hiki, mfasiri anashauriwa aisome matini chanzi kwa mara ya mwisho huku
akipigia mstari au kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi
na misemo muhimu ya matini chanzi kama vile, methali, nahau maneno ya
kitamaduni yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au
kuyaandika katika kidaftari kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri
kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri lakini pia
kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri.
Hayo
ndiyo mambo ambayo, mfasiri anatakiwa kuyazingatia kabla hajaanza
mchakato wa kutafsiri. Hivyo basi, sasa tugeukie upande wa pili ambao
ni:
[b] Mambo ya kuzingatia wakati wa mchakato wa kutafsiri.
? Maandalizi ya kutafsiri
Katika
hatua hii, mfasiri anatakiwa kufahamu vizuri maudhui ya matini chanzi,
ujumbe wake, mtindo wa matini na kuwekea alama sehemu zenye utata au
zisizoeleweka vizuri, anashauriwa kupigia mstari au kuandika katika
kidaftari kidogo msamiati, istilahi na misemo muhimu ya matini chanzi
kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni yasiyotafsirika, majina
maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari kidogo
ili iwe rahisi kwa mfasiri kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza
kutafsiri lakini pia kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri
au kuyatolea ufafanuzi zaidi katika tafsiri yake.
? Uchambuzi wa matini chanzi
Katika
hatua hii, mfasiri anatakiwa kuchunguza kwa makini maneno, methali,
nahau, misemo pamoja na maelezo mengine ya matini chanzi aliyoyaandika
au kuyapigia mstari katika hatua ya maandalizi na kuyatafutia visawe
vyake katika lugha lengwa, hapa mfasiri anashauriwa kutumia marejeo
mbalimbali kama vile, kamusi, ensiklopedia, orodha ya msamiati na
istilahi mpya.
Mfasiri anatakiwa kuwa na shajara au
daftari dogo kwa ajili ya kuandika na kuhifadhi maneno na maelezo muhimu
ya matini chanzi na visawe vyake, visawe vinavyoonekana kufaa
viorodheshwe vizuri ili iwe rahisi kuvirejelea wakati wa kutafsiri,
vilevile mfasiri kama ataona kuwa matini chanzi ni ndefu sana,
anashauriwa kuigawa matini hiyo katika sehemu ndogondogo kama vile,
sura, aya au sentensi na kuanza kushughulikia sehemu moja baada ya
nyingine.
? Uhawilishaji
Uhawilishaji ni
uhamishaji wa mawazo kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa, au
uhamishaji wa mawazo au ujumbe kutoka matini asilia kwenda matini ya
tafsiri. Hii ina maana kuwa katika hatua hii, visawe vya kisemantiki
[kimaana] vya matini chanzi vilivyobainishwa katika hatua ya uchambuzi
huamishwa katika matini lengwa [kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa]
na kupangwa vizuri kisarufi na kimantiki ili fasiri hiyo iwe na maana
kwa wasomaji wake.
? Kusawidi /Kuandaa rasimu ya kwanza ya tafsiri.
Katika
hatua hii, mfasiri huandika rasimu yake ya kwanza ili kupata picha
fulani ya matini aliyoikusudia, katika uandaaji wa rasimu ya kwanza, kwa
kufanya hivi, mfasiri anaweza kugundua kuwa anahitaji taarifa zaidi
tofauti na alizozipata katika hatua ya uchambuzi, na hivyo kulazimika
kuchunguza zaidi matini chanzi na hata kupekua zaidi na zaidi marejeo
yake aliyoyaandaa kwa kuyatumia katika tafsiri. Jambo la kuzingatia,
mfasiri anatakiwa wakati akihamisha mawazo au ujumbe azingatie umbo na
lengo la matini chanzi ili kutoathiri tafsiri yake.
? Kudurusu / kuipitia rasimu ya kwanza
Baada
ya kusawidi rasimu ya kwanza, mfasiri anatakiwa kuivundika rasimu yake
ya tafsiri kati ya juma moja hadi mawili baada ya kukamilika kwake na
kuanza kuidurusu/ kuipitia rasimu hiyo kwa jicho la kihakiki zaidi na
kuangalia kama kuna makosa ambayo yamejitokeza katika rasimu yake au la
na kuyafanyia marekebisho pale inapobidi.
? Kusomwa kwa rasimu ya tafsiri na mtu/watu wengine
Baada
ya mfasiri kuipitia rasimu yake ya kwanza, na kuifanyia masahihisho kwa
makosa yaliyojitokeza, anatakiwa kuwapa watu wengine waidurusu rasimu
hiyo iliyofanyiwa marekebisho ili waipitie tena na kuirekebisha, hivyo
basi wasomaji hao wanaweza wakahakiki,wakashauri, n.k. Wasomaji hawa
husaidia kuona kama tafsiri iko sahihi, inaeleweka na ina mtiririko
mzuri wenye mantiki.
? Usawidi /Kuandika rasimu ya mwisho
Baada
ya kupata maoni kutoka kwa wasomaji wa pili, mfasiri anaweza kuyatumia
maoni, mapendekezo na maelekezo yao kusahihisha tena tafsiri yake na
hatimaye kuandaa na kutoa rasimu ya mwisho ambayo itakuwa tayari kwa
kusomwa na wasomaji.
Njia / mbinu za Tafsiri
Zipo njia mbalimbali ambazo hutumika katika kutafsiri, baadhi ya njia hizo ni kama vile:
(i) Tafsiri ya neno kwa neno. [Word to word translation]
(ii) Tafsiri sisisi.[ Literal translation]
(iii) Tafsiri ya kimaana/uwazi.[ Semantic translation]
(iv) Tafsiri ya kimawasiliano.[Communicative translation]
(i) Tafsiri ya neno kwa neno [Word to word translation]
Hii
ni aina ya tafsiri ambayo mofimu na maneno hufasiriwa yakiwa pweke
pweke kwa kuzingatia maana zake za msingi bila kujali muktadha. Katika
aina hii ya tafsiri mpangilio wa mofimu na maneno wa lugha chanzi
hubakia vilevile bila kubadilika. Na kwa kawaida matini inayotafsiriwa
huandikwa chini ya matini ya lugha chanzi. Tazama mifano ifuatayo ya
tafsiri ya neno kwa neno:
Kiswahili: Alisoma hadi asubuhi
Kingereza: He/past/study/until/morning
Kiswahili: Alikimbia mpaka ofisini kwake
Kingereza: He/past/run/until/office/his
Kiswahili: Anasoma kitabu changu
Kingereza: He/present/book/my
Kiswahili: Walikula chakula chote
Kingereza: They/past/eat/food/all
Umuhimu
wa njia hii, humsaidia mtu kuelewa muundo wa lugha chanzi na jinsi
lugha chanzi inavyofanya kazi, kaina hii ya tafsiri hutumiwa na
wataalamu wa lugha kuonesha namna maumbo au muundo wa lugha chanzi
ulivyo, lakini mapungufu yake ni kuwa, aina hii ya tafsiri huwa haitoi
maana inayokusudiwa kwa uwazi zaidi.
(ii) Tafsiri sisisi [ Literal translation]
Hii
ni aina ya tafsiri ambayo maneno hufasiriwa yakiwa pweke pweke kwa
kuzingatia maana za msingi katika lugha chanzi bila kujali sana muktadha
lakini ni tafsiri inayofuata mfumo wa kisarufi hasa kipengele cha
kisintaksia ya lugha lengwa. Ebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kingereza: He was taken at the Central Police Station
Kiswahili: Alipelekwa kwenye kituo cha kati cha police.
Badala ya kuwa: Alipelekwa kituo kikuu cha polisi
(iii) Tafsiri ya kisemantiki/maana au uwazi [Semantic Translation]
Hii
ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri huegemea zaidi kwenye lugha chanzi.
Katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri kila neno katika sentensi
jinsi lilivyo lakini kwa kufuata sarufi hususani vipengele vya
kisemantiki na kisintaksia ya lugha chanzi. Inaitwa tafsiri ya
kisemantiki kwa sababu, mfasiri anapofasiri hutakiwa kuweka mkazo kwenye
maana ya matini kama ilivyokusudiwa na mwandishi wa matini chanzi.
Katika
aina hii ya tafsiri, masahihisho au urekebishaji wa neno au jambo
lolote unalodhani limekosewa haliruhusiwi isipokuwa unaweza kuweka hayo
marekebisho au ufafanuzi katika tanbihi. Sasa tuangalie baadhi ya mifano
ya aina hii ya tafsiri:
Kiswahili: Alikwenda mpaka hospitali
Kingereza: He went up to hospital
Kingereza: Jane married John
Kiswahili: Jane alimwoa John
Aina
hii ya tafsiri, ina faida kubwa katika ukuaji wa lugha lengwa kwa
kuingiza miundo ya misemo kutoka lugha chanzi, mathalani, lugha ya
Kiswahili imepokea miundo mipya ya misemo kutoka lugha ya Kingereza,
baadhi ya miundo hiyo ni kama vile:
Kiswahili: Usiku mwema ? kutoka Kingereza: Good night
Kiswhili: Mabibi na mabwana ? kutoka Kingereza: ladies and gentlemen
Kiswahili: Wako mtiifu ? Kutoka Kiingereza: Yours Sincerel
Kiswahili: Naomba nichukue nafasi hii.. ? Kutoka Kiingereza: May I take this opportunity…
[Tazama pia Mwansoko na wenzake: 2006]
(iv) Tafsiri ya kimawasiliano/ huru [Communicative Translation]
Hii
ni aina ya tafsiri inayomlenga msomaji [hadhira] wa matini lengwa,
ambaye katika aina hii ya tafsiri hatarajii kukutana na ugumu wowote
katika matini atakayoisoma, bali hutarajia kukutana na tafsiri nyepesi
ya dhana za kigeni katika utamaduni na lugha yake kwa kadiri
itakavyoonekana. Hivyo basi, mfasiri wa aina hii ya tafsiri yuko huru
kutafuta maneno na mafungu ya maneno yanayolingana na maneno, methali,
nahau, utamaduni na mazingira ya lugha lengwa, pamoja na kuwa tafsiri ya
kimawasiliano kufuata sarufi ya lugha lengwa ni lazima pia ifuate
utamaduni, mazingira na historia ya jamii ya lugha lengwa. Tuangalie
mifano ifuatayo:
Kingereza: Jane married John
Kiswahili: John alimwoa Jane
Kingereza: No need to cry over spilt milk
Kiswahili: Maji yakimwagika hayazoleki
Kiingereza: What comes around goes arround
Kiswahili: Mla vya watu, naye vyake huliwa.
Kiswahili: Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
Kiingereza: A friend in need is a friend in need
Kiswahili: Bahati haiji mara mbili
Kiingereza: Golden chance never comes twice
Aina
hii ya tafsiri hulenga kutoa athari ile ile au inayokaribiana kwa
hadhira ya matini lengwa kama ilivyo kwa hadhira ya matini chanzi[
matini asilia], hii ni aina ya tafsiri ambayo hutumika sana kufasiri
mawazo ya kigeni katika lugha na mazingira mapya, mawazo ambayo huelezwa
katika misingi ya lugha, utamaduni na mazingira yanayoeleweka kwa
hadhira ya matini lengwa.
Ebu tuangalie baadhi ya
mifano tuliyoiangalia katika tafsiri ya Kisemantiki [maana] tunavyoweza
kutafsiri katika njia ya tafsiri ya kimawasiliano:
Kiingereza Kiswahili
Good night Lala salama
Ladies and Gentlemen Ndugu zangu
Yours Sincerely Ni mimi
May I take this opportunity to… Naomba mnisikilize
Hivyo
basi, katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hutafuta methali au misemo
inayopatikana katika lugha lengwa inayohusiana au kukaribiana na ile ya
lugha chanzi. Ebu jaribu kutafsiri misemo/methali zifuatayo ya lugha ya
Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza:
Adhabu ya kaburi aijuaye maiti
Asiyekubali kushindwa si mshindani
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa
Chema chajiuza kibaya chajitembeza
Dua la kuku halimpati mwewe
Bandubandu humaliza gogo
Jogoo wa shamba hawiki mjini
La kuvunda halina ubani
Mtegemea cha nduguye hufa masikini
Faida
ya aina hii ya tafsiri, humfanya mfasiri kuwa huru kutumia maneno au
mafungu ya maneno ambayo huweza kutoa athari ile ile au inayokaribiana
na maneno au mafungu ya maneno katika matini ya lugha chanzi, lakini
mapungufu ya aina hii ya tafsiri huweza kutokea iwapo mfasiri ataamua
kuegemea mno kwenye mawazo, historia, mazingira au itikadi ya lugha
lengwa. Ebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kingereza: The Merchant of Venice
Kiswahili: Mabepari wa Venisi
Ukiangalia
mfano huo utaona kuwa, The Merchant of Venice, tamthiliya iliyoandikwa
na William Shakespeare, ingefaa pia kufasiriwa kuwa, Wafanyabiashara wa
Venisi, lakini Mwalimu J.K Nyerere aliamua kuifasiri kuwa, Mabepari wa
Venisi kutokana na kuwa Nyerere ndiye mwasisi wa itikadi ya Ujamaa
nchini Tanzania, hivyo aliegemea katika itikadi kufasiri.
Hivyo
basi, mtu anapokuwa anafanya kazi ya kufasiri, maandishi yo yote kutoka
lugha moja kwenda lugha nyingine atajikuta akiangukia katika moja wapo
ya njia tulizozijadili hapo juu, lakini ikumbukwe tafsiri ya neno kwa
neno ni nadra sana kutumiwa na wafasiri wengi, na njia hizo huweza
kuingiliana katika matini moja ya tafsiri.
Ukalimani [Interpritation]
Ukalimani ni nini?
Ukalimani
imefasiliwa kuwa ni, uhusishaji wa kuhamisha maana kutoka lugha moja
(lugha chanzi) kwenda lugha nyingine (lugha lengwa) katika mazungumzo.
Hivyo basi tunaweza kusema pia, ukalimani ni hali ya mtu kuhamisha
mawazo ya kinachozungumzwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine
katika mazungumzo. Hii ina maana kuwa ukalimani ni lazima uhusishe pande
mbili, upande wa kwanza sharti awepo mtu anayezungumza lugha fulani na
upande mwingine kunakuwa na mtu ambaye anasikiliza hicho
kinachozungumzwa na kuyarudia hayo yanayozungumzwa kwa kutumia lugha
nyingine tofauti na ile iliyotumiwa na mazungumzaji wa kwanza.
Hivyo
basi, ukiangalia, maana hiyo tuliyoiangalia utaona kuwa, ukalimani ni
taaluma inayohusu mazungumzo wakati tafsiri yenyewe uhusu maanadishi,
kwa maana hiyo huwa tunatafsiri maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha
nyingine na tunakalimani mazungumzo kutoka lugha moja kwenda lugha
nyingine.
Ukalimani ulianza pale ambapo mataifa mbalimbali yenye
kuzungumza lugha tofauti tofauti yalipoanza kuingiliana na kushirikiana
katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa, kichumi na kiutamaduni,
kwa mfano ujio wa wageni Afrika Mashariki kama vile Waarabu, Wajerumani
na Waingereza ili waweze kuwasiliana na wenyeji wao waliambatana na watu
ambao walikuwa wakiwatumia kama wakilamani wao.
Kwa sasa hivi
ukalimani umekuwa kama taaluma muhimu, ukalimani unafanyika katika
mahakama, kanisani, katika mikutano ya kimataifa, mahubiri ya kidini,
n.k na kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna vifaa
maalumu ambayo hutumika kukalimani mazungunzo kutoka lugha moja kwenda
lugha nyingine, ambayo huvaliwa masikioni katika kumbi za mikutano. Na
sasa ni taaluma inayofundishwa katika shule za sekondari na elimu ya juu
kama ilivyo kwa tafsiri kutokana na umuhimu wake.
Mkalimani ni
mtu muhumi sana katika kufanikisha mawasiliano kwa watu wanaotumia lugha
mbili tofauti, au lugha inayotumika katika eneo hilo msikilizaji
haielewi na haijui na ndiyo maana utakuta wakalimani wakihitajika
mahakamni, mikutano ya kimataifa, katika mahubiri ya kidini au mahali
popote pale ambapo wazungumzaji hawawezi kuelewana kwa kuwa wanatumia
lugha tofauti.
Sifa za mkalimani bora
? Awe mtu anayezielewa lugha chanzi na lugha lengwa vizuri
? Awe ni mtu ambaye ameishi pande zote za lugha anazozikalimani ili kuelewa mila na desturi za watumiaji wa lugha hizo.
?
Awe stadi wa ukalimani, hapa inatakiwa awe na uhodari wa kukalimani,
kuzungumza vizuri, maneno kusikika, awe na uwezo wa kukalimani neno kwa
neno au sentensi na sentensi, kutumia ishara zinazoambatana na ishara za
mzungumzaji wa lugha chanzi na hata kutumia mtindo anaodhani unaweza
kuwavutia wasikilizaji wake.
? Muadirifu, ambaye hawezi kupotosha
au kubadili ukweli wa kinachozungumzwa, nah ii ni muhimu kwa sababu
wakalimani hutumika hadi mahakami hivyo kama si mwadirifu huweza
kuufanya upande mmoja ukakosa haki inayostahiri.
? Asiwe mbaguzi,
hapa ina maana mkalimani asiamue kupotosha ukweli wa kile
kinachozungumzwa kwa kuwa tu kinaendana kinyume na itikadi yake ya
kisiasa, kidini, kiutamaduni, n.k. wala asiangalie jinsia ya mtu umri au
hali ya mtu anayemfanyia ukalimani.
Mambo ya kuzingatia katika Ukalimani
Kwa
ujumla yapo mambo kadha wa kadha, ambayo mkalimani anatakiwa
kuyazingatia anapotaka kufanya ukalimani, mambo hayo tunaweza kuyagawa
katika makundi mawili, ambayo ni:
1. Kabla ya kuanza ukalimani
Katika hatua hii, mkalimani anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
(a)
Awe na uelewa mzuri wa lugha zote anazotaka kukalimani, hapa tuna maana
kuwa awe na uwezo wa kuzungumza na kuelewa lugha chanzi na lugha lengw,
hii itasaidia mkalimani kutopotosha kile kinachozungumzwa na
mzungumzaji wa lugha chanzi.
(b) Awe anaijua historia na utamaduni wa jamii zote mbili, yaani ile ya lugha chanzi na ile ya lugha lengwa.
(c)
Kama ni ukalimani rasmi, ni vizuri kwa mkalimani akamjua mzungumzaji wa
lugha chanzi, ni vema pia ukafanya naye mazungumzo kidogo ili kumzoea,
na kutambua vionjo vyake ili iwe rahisi kwa mkalimani pindi atakapokuwa
anafanya ukalimani asionekane kama mgeni.
(d) Vilevile ni muhimu
kwa mtu anayekalimani, akawa na uelewa mzuri wa mada inayozungumzwa, hii
itamrahisishia mkalimani katika ukalimani wake.
2. Katika ukalimani wenyewe
Mkalamani
anapokuwa amesimama mbele ya hadhira [wasikilizaji] pamoja na
mzungumzaji wa lugha chanzi kwa ajili ya kuanza ukalimani, anatakiwa
kuzingatia mambo yafuatayo:
(a) Kuwa makini katika kusikiliza
kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa lugha chanzi ili kuepuka kuachwa
mahali na kuepuka kumuomba mzungumzaji kurudia mara kwa mara.
(b)
Itambue hadhira ya lugha lengwa, ni watu wa namna gani, wana kiwango
gani cha elimu, ni wasomi wa kawaida au waliobobea, ni watu wa jinsia na
umri gani,? Hii itakusaidi kujua aina ya msamiati na miundo ya tungo
utakayoitumia, kama iwe rahisi au migumu kutokana na hadhira yako
ilivyo.
(c) Tumia mitindo unayodhani itaeleweka vema na hadhira/
wasikilizaji wa lugha lengwa, kwa mfano kama hadhira yako ni vijana,
jaribu kutumia mitindo inayopendwa na vijana, kama wasikilizaji wako ni
watu rasmi na we huna budi kuwa rasmi.
(d) Weka mkazo sehemu
ambazo mzungumzaji wa lugha chanzi anaweka mkazo ili kuepuka utofauti
yako na mzungumzaji wa lugha chanzi, na hata kuepuka kuathiri lengo la
mzungumzaji wa lugha chanzi.
(e) Unatakiwa pia kutumia ishara
zinazotumiwa na mzungumzaji wa lugha chanzi, hii itawafanya wasikilizaji
waamini kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa lugha chanzi ndiyo
kilekile kinachozungumzwa na mkalimani.
(f) Usiwe muda mwingi
unamtazama mzungumzaji wa lugha chanzi na kusahahu kuitazama hadhira
yako, hivyo unatakiwa kuitazama hadhira yako ili kugundua kama wako
pamoja na wewe au kuna sehemu hawajakuelewa ili uweze kuwafafanulia
zaidi.
(g) Muombe mzungumzaji wa lugha chanzi kurudia sehemu
unayodhani hujaisikia au hujaielewa vizuri, kwani ni makosa kwa
mkalimani kukalimani sehemu au jambo ambalo hukulisikia vizuri au
kulielewa.
Hivyo basi hayo ndiyo mambo muhimu ambayo mkalimani
anatakiwa kuyazingatia anapokuwa anafanya ukalimani. Jambo la
kuzingatia, mkalimani hutakiwa kuingiza hisia zako unapokuwa anafanya
ukalimani. na ukalimani mzuri unawezekana kwa kiwango ambacho mila na
desturi zote yaani za lugha chanzi na lugha lengwa zinalingana ama
kushabihiana.
Dhima za Tafsiri na Ukalimani
Tafsiri na Ukalimani ina dhima zifuatazo:
? Hutuwezesha kujifunza lugha tofauti.
Kati
ya mazoezi mazuri anayoweza kutumia mtu katika kujifunza lugha
nyingine, basi zoezi la kutafsiri au kukalimani mara kwa mara humsaidia
mtu kujifunza lugha kwa urahisi zaidi, kwani kwa kufanya tafsiri ya mara
kwa mara kutamsaidia mtu kugundua miundo na vipengele mbalimbali vya
lugha na jinsi vinavyofanya kazi katika lugha anayojifunza.
? Hutumika kama njia ya mawasiliano.
Kutokana
na maingiliano ya mataifa mbalimbali yanayotumia lugha tofauti tofauti,
tafsiri hutumika kurahisisha mawasiliano baina ya makundi ya watu
wanaotumia lugha tofauti tofauti, hutumika kutolea maelezo ya kibiashara
kama vile maelekezo ya jinsi ya kutumia bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa nje au zinazouzwa nje ya nchi, katika matangazo ya
kitalii ili kuwavutia watalii kutoka mataifa mbalimbali, vilevile
hutumika katika vyombo vya habari, tafsiri pia inatumika katika nyaraka
rasmi, mikataba, vitabu vya ziada na kiada, lakini pia ukalimani
hulahisisha mawasiliano miongoni mwa watu wanaozungumza lugha tofauti.
? Tafsiri na Ukalimani hutumika kueneza utamaduni.
Tafsiri
imekutanisha lugha na tamaduni mbalimbali duniani na kusababisha
tamaduni na lugha hizo kuathiriana, kwa mfano mara baada ya waarabu
kuingia Afrika Mashariki na vitabu mbalimbali vya Kiarabu na Kiislamu
kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ilisababisha utamaduni wa Kiswahili
kuathiriwa na utamaduni wa Kiarabu na Kiislamu kutoka na kuiga kwa mambo
mengi kutoka huko, lakini pia hata walipokuja wazungu na kutafsiri
vitabu vyao vya kifasihi, kutafsiriwa kwa Biblia, n.k. ilisababisha pia
utamaduni wa Mswahili kuathiriwa na utamaduni wa Ulaya.
? Tafsiri na Ukalimani ina dhima ya kuwasilisha ujumbe wa manufaa kwa watu ambao hawafahamu lugha chanzi [lugha asilia]
Changamoto/ mapungufu katika tafsiri na Ukalimani
Mfasiri
katika kazi yake ya kufasiri hukumbana na changamoto mbalimbali, ambazo
huweza kusababisha tafsiri kuwa na mapungufu ya hapa na pale. Baadhi ya
changamoto au mapungufu hayo ni kama vile:
(i) Tofauti za kiisimu kati ya lugha chanzi na lugha lengwa.
Tofautui
za maumbo, miundo na maana kati ya lugha ya Kiswahili na lugha ya
Kingereza wakati mwingine husababisha matatizo au upungufu katika
tafsiri na ukalimani. Kwa mfano maumbo ya vitenzi vya Kiingereza
huruhusu kauli nyingi elekezi kutoonesha umoja au wingi wa wahusika wala
majina ya vitu mahususi vinavyoambatana na maelekezo yanayotolewa
tofauti maumbo ya vitenzi vya Kiswahili ambavyo huonesha umoja na wingi
wa wahusika na hata kuwa na majina ya vitu husika, tazama mifano
ifuatayo kama ilivyotolewa na, Mwansoko [2006]
Kingereza Kiswahili
No parking ? Usiegeshe gari hapa [je kisichoruhusiwa kuegeshwa ni gari tu?]
No Smoking ? Usivute sigara[ Je ni sigara tundiyo hairuhusiwi kuvutwa?]
Arrivals ? Wanaowasili
Departures ? Wanaosafiri
Vilevile tofauti za maana kati ya lugha ya Kingereza na Kiswahili huweza kuathiri tafsiri au ukalimani, mathalani:
Kiswahili Kingereza
Wasiojiweza ? Disabled [Siyo wote wasiojiweza ni walemavu]
[na siyo walimavu wote hawajiwezi]
Wezi wa mifukoni? Pickpockets [Hawaibi kwenye mifuko, wanaiba kutoka mifukoni]
(ii) Tofauti za mitindo kati lugha chanzi na lugha lengwa
Tofauti
za mitindo ya uzungumzaji pia, huweza kuathiri tafsiri na ukalimani na
hii ni kwa sababu unaweza kukuta kuna mitindo fulani inaweza kutumika
katika muktadha fulani lakini ikishindwa kupata tafsiri katika lugha
nyingine katika muktadha ule ule.mathalani:
Kingereza: Kiswahili
(i) Thou shalt not steal [mtindo wa kidini] ? Usiibe
Do not steal [mtindo wa kawaida] ? Usiibe
(ii) Lend me your ears [mtindo wa kishairi] ? Naomba mnisikilize
May I have your attention [kawaida] ? Naomba mnisikilize
Tafsiri
zote tulizoziangalia katika mfano wa (i) na (ii) zimetoa maana au
taarifa ili ile iliyomo katika matini chanzi lakini tafsiri hizo
hazikuzingatia mtindo wa lugha iliyotumika katika matini chanzi.
(iii) Tofauti za kitamaduni kati ya lugha chanzi na lugha lengwa
Tofauti
za kiutamaduni, yaani taofauti za kimila, desturi na mazingira ya
watumiaji wa lugha chanzi na lugha lengwa huweza kufanya tafsiri au
ukalimani kuwa mgumu, kwa mfano, katika utamaduni wa Waingereza wana
milo minne wakati Waswahili wana milo mitatu na hii hupelekea kuwa
vigumu kupata dhana za milo ya hiyo ya Waingereza katika dhana ya
Kiswahili. Mfano:
Waingereza wana: Waswahili wana:
Breakfast ------------------ Kifungua kinywa
Lunch …………………... Chakula cha mchana
High tea ……………………?
Dinner ……………………Chakula cha jioni
Supper …………………….?
Kwa
hiyo ukiangalia mifano hiyo, utaona kuwa, high tea na supper kuzipata
dhana zake katika lugha ya Kiswahili ni ngumu kutokana na kutokuwa na
utamaduni wa kuwa na milo kama hiyo kwa siku. Lakini pia inakuwa vigumu
kupata tafsiri ya vyakula kama vile ugali, makande katika lugha ya
Kiingereza kutokana na kutokuwa na vyakula vya aina hiyo.
(iv) Tofauti za kiitikadi kati ya lugha chanzi na lugha lengwa
Tofauti
za kiitikadi pia huweza kuathiri tafsiri na ukalimani, na hii ni kwa
sababu, utakuta wafasiri wengi hususani waandishi wa habari kuegemea
katika itikadi zaidi, kwa mfano:
Kingereza Kiswahili
Bussnessman ? mlanguzi [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na itikadi
ya ujamaa]
mfanyabiashara [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na
itikadi ya ubepari]
Freedom fighter ? wapigania uhuru [Tafsiri ya vyombo vya habari vya
Tanzania wakati wa kupigania uhuru]
Magaidi [Tafsiri ya idhaa ya BBC na Radio za Afrika
Kusini wakati huo]
Hivyo
basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, ukalimani mzuri unawezekana
kwa kiwango ambacho mila na desturi zote yaana za lugha chanzi na lugha
lengwa zinalingana ama kushabihiana.
Na kutokana na umuhimu wa
taaluma hii ya tafsiri na ukalimani, serikali kupitia Baraza la
Kiswahili la Taifa Bakita [BAKITA] imeanzisha idara maalumu ya Tafsiri
na Ukalimani, na idara hiyo ina majukumu yafuatayo:
? Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mbalimbali kwa masharika, idara, wizara, balozi na watu binafsi.
?
Kuratibu na kutoa huduma za ukalimani kwenye mikutano ya kitaifa na
kimataifa na katika shughuli za masharika, makampuni na watu binafsi.
? Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na asasi mbalimbali au wafasiri wa nje.
? Kutoa ushauri kuhusu masula ya tafsiri na ukalimani.
MAZOEZI
? Zoezi la kwanza
Fasili matini ifuatayo kwenda lugha ya Kiingereza:
MTO
(Siku ifuatayo, asubuhi. Ngoswe na Mitomingi wako kazini. Wanafika nyumba moja).
MITOMINGI: Hodi! Hodi! Wenyewe! (Kimya, hakuna sauti itokayo). Hodi wenyewe
(Kimya) Labda hawajaamka.
NGOSWE: Kama bado wamelala tuwaache kwanza tuwarudie baadaye.
MITOMINGI: Mimi naona itakuwa shida shida kwani nyumba za hapa zimesambaa
mno.hebu nibishe tena.hodi! hodi! Wenyewe mpo?(Akinyamaza na
kunapita kimya. Punde mlango wafunguka na kipande cha
mwanamke chatokeza). Habari za asubuhi mama?
MAMA: Salama, mwaonaje?
MITOMINGI
NGOSWE Hatujambo
MAMA: Sijui niwasaidie nini akina baba?
MITOMINGI: Mwenyewe yupo sijui?
MAMA: (Akitazama chini mwenye huzuni anatingisha kichwa). Hayupo
MITOMINGI: Katoka kitambo?
MAMA: (Akimtazama Mitomingi kwa jicho kali). Ni marehemu.
MITOMINGI: (Amtazama Ngoswe ambaye kainamisha kichwa na wote wanamtazama
kwa jicho la huruma). Pole mama.
NGOSWE: Pole mama.
MAMA: Nimekwisha poa.
MITOMINGI: Samahani mama , hata sikufahamu.
MAMA: Sio neno baba sio kosa lako.
MITOMINGI: Mungu mkubwa.
MAMA: Nifanyeje; kazi ya Mungu haina dosari. (Ananyamaza kwa kitambo). Je
niwasaidie nini?
MITOMINGI: Jambo moja dogo tu. Samahani kama nitakusumbua maana kwanza ni
asubuhi tena yenyewe ni msiba,
MAMA: Sio kitu baba.
MITOMINGI: Nadhani umepata kumsikia Balozi Mitomingi.
MAMA: Nimemsikia lakini kumwona bado.
MITOMINGI: Basi mama, huyo Mitomingi, Ngengemkeni Mitomingi ndiye mimi.
MAMA: (Kwa mshangao): Karibuni ndani mpumzike
MITOMINGI: Hatukai sana mama.
MAMA: Basi ngoja niwatolee viti make. (Aingia ndani na kutoka na viti viwili
kuwapatia wageni. Yeye aketi chini).
MITOMINGI: Mama!
MAMA: Baba!
MITOMINGI: Nadhani una habari juu ya kuhesabu watu.
MAMA: (Kwa mshangao): Kuhesabu watu?
MITOMINGI: Ndiyo kuhesabu watu.
MAMA: Kuhesabu watu! (Akitingisha kichwa) Hapana.
MITOMINGI: Balozi wenu hakuwajulisha?
MAMA: Hata kidogo.
MITOMINGI: Kweli?
MAMA: Kwani Tambitambi naye mtu yule!
Pombe na yeye ni pete na chanda!
Hajali Balozi wake wala nyumba yake.
MITOMINGI: Ni sawa usemayo mama. Tambitambi yule akili hazimtoshi. Tumefika
kwake wala hajulikani aliko!
MAMA: Kama kuna wanaume mabwege yule ametia for a.
MITOMINGI: Usizidi kunambia mama, Tambitambi mambo yake hakuna
asiyeyafahamu…. Sasa mama!....
MAMA: Ndiyo baba.
MTOMINGI: Sisi kama utuonavyo tuko shughulini, shughuli hiyo si nyingine bali hiyo
niliyoisema sasa hivi kuhesabu watu. Na huyu kijana ndiye karani
mwenyewe ahusikaye. Ingekuwa bora kama wewe na wanao wote
mngetoka nje ili tufanye kazi yetu.
MAMA: Sasa baba mbona itakuwa vigumu.
MITOMINGI: Kwa vipi?
MAMA: Sasa baba utahesabu vipi?
MITOMINGI: Kwa nini?
MAMA: Kama utatuhesabu wewe basi u mchawi.
MITOMINGI: Mbona sikuelewi!
MAMA: Mchawi ndiye anayehesabu watoto wa wenzake ili awaroge. Sasa wewe
umchawi? Hata kama u mchawi siwezi kukubali utuhesabui maana
siwezi kujua nia yako ni mbaya au nzuri.
MITOMINGI: Mtu akuwaniae uovu haji kweupe.
MAMA: Sawa usemayo baba.
NGOSWE: Sasa mama hebu walete wanao na yeyote yule aliye ndani.
MAMA: Wanangu hawapo wamekwenda shamba kuwania mpunga.
NGOSWE: Wote?
MAMA: Ndiyo.
NGOSWE: Ndio kusema hakuna kiumbe hata kimoja?
MAMA; Yuko mke mwenzangu.
NGOSWE; Tuitie.(Mama anasimama kwa unyonge na kuingia ndani. Anarudi peke
yake baada ya muda mfupi). Yu wapi?
MAMA: Aja (Punde mama mwingine atokea. Yu kariby rika moja na mama wa
kwanza isipokuwa huyu mbichimbichi).
MITOMINGI: Habari mama?
NGOSWE: (Wakati huohuo) Shikamoo.
MAMA WA PILI: Nzuri (Atazama chini kwa aibu huku akiketi).
NGOSWE: (Akimtazama mama wa kwanza). Basi; hakuna mtu mwingine ndani?
MAMA WA PILI: (Akikataa kwa kichwa)
MITOMINGI: (Kwa mama wa kwanza). Lakini nyie wanawake mbona waoga sana!
Hivyo mnataka kuniambia motto wa mgongoni anaweza kwenda
kuwania mpunga? (Mama agutuka). Hebu niambie mwanao mchanga
yu wapi?
MAMA WA KWANZA: Sina mtoto mchanga.
MITOMINGI: Hivyo mama wasema kweli?
MAMA WA KWANZA: Haki vile.(Mara kwasikika sauti ya mtoto akilia ndani ya
nyumba).
MITOMINGI: Na huyo anayelia kama si mtoto ni nini/ (Mama ainuka wakawaka na
kuingia ndani kwa aibu. Muda wapiti na harudi). Mama! Njoo basi
tumalize shughuli. Usijali mambo ya motto kulia, ni jambo la kawaida.
(Mama atokea amepakata mtoto mchanga. Aketi chini na sasa uso wake
umejaa hasira na chuki)…
[Imenukuliwa kutoka, Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. Uk 13-15]
? Zoezi la pili
1. Linganisha na linganua kati ya taaluma ya tafsiri na ukalimani.
2. (a) Tafsiri sentensi zifuatazo kwenda lugha ya Kiingereza
(i) Dua la kuku halimpati mwewe
(ii) Bandu bandu humaliza gogo
(iii) La kuvunda halina ubani
(iv) Mla vya watu naye vyake huliwa
(v) Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
(b) Ni njia gani umetumia katika tafsiri ulizotoa hapo juu, unadhani ni kwa nini?
??Zoezi la tatu
1. [a] Kwa kutumia mifano, fafanua istilahi zifuatazo:
[i] Matini chanzi
[ii] Matini lengwa
[iii] Lugha chanzi
[iv] Lugha lengwa
[b] Tafsiri sentensi zifuatazo kwenda lugha ya Kiswahili
(i) All that glister is not gold
(ii) Looser casn't be a chooser
(iii) When you make your bed you must lie on it
(iv) There is no incense for something rotting
(v) When in Rome do, do as Romans do
(b) Ni njia gani umetumia katika tafsiri hizo ulizotoa hapo juu, unadhani ni kwanini?
2. "Mfasiri au mkalimani hukabiliana na changamoto mbalimbali katika kufanikisha kazi
yake." Huku ukitumia mifano thibitisha kauli hiyo.
MAREJEO
Cartford [1995] A linguistic Theory Translation
Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na
Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam
Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press
Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.
Oxford University Press Dar-es-salaam
Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.
D.S.M
TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam
TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2011
www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2011
www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2011
Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo
Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla
Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.
William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere
Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere
Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa
Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton
Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman
AN ONLINE PLATFORM THAT PROVIDES EDUCATIONAL CONTENT,SYLLABUSES, STUDY NOTES/ MATERIALS ,PAST PAPERS, QUESTIONS & ANSWERS FOR THE STUDENTS,FORM I--VI ,RESITTERS,QT, ADULT LEARNERS, COLLEGE STUDENTS, PUPILS, TEACHERS, PARENTS,TEACHERS OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND WORLDWIDE.YOU ARE WELCOME TO SHARE YOUR KNOWLEDGE AND IDEAS.ENJOY MASATU BLOG.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE. "LEARN.REVISE.DISCUSS".Anytime, Anywhere.
- HOME
- UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ?
- MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI
- HOW TO IMPROVE YOUR MEMORY
- ONLINE LEARNING & DISTANCE LEARNING ( E--LEA...
- O-LEVEL & A--LEVEL SYLLABUS
- FORM FOUR ( F 4 )--SUBJECTS---TANZANIA
- FORM TWO ( F 2 )--SUBJECTS---TANZANIA
- FORM ONE ( F 1 )-- SUBJECTS---TANZANIA
- FORM FIVE( F 5 ) AND SIX ( F 6 )--SUBJECTS ---TANZANIA
- FORM THREE ( F 3 ) SUBJECTS----TANZANIA
- STANDARD 1 & 2 SUBJECTS / MASOMO YA DARASA 1 & 2-...
- STANDARD 3 & 4 SUBJECTS / MASOMO YA DARASA 3 & 4...
- STANDARD 5, 6 & 7 SUBJECTS / MASOMO YA DARASA...
Friday, March 21, 2014
Monday, March 17, 2014
Monday, March 10, 2014
JAPHETH FROM WIKIPEDIA. THE FREE ENCYCLOPEDIA
Japheth
From Wikipedia, the free encyclopedia
For other uses, see Japheth (disambiguation).
This article needs additional citations for verification. Please help improve this article by adding citations to reliable sources. Unsourced material may be challenged and removed. (January 2010) |
Japheth | |
---|---|
Japheth, as depicted in Promptuarii Iconum Insigniorum (c. 1553)
|
|
Born | 1557 AM (date disputed)[1] |
Children | Gomer Magog Madai Javan Tubal Meshech Tiras |
Parents | Noah |
Contents
Order of birth
Japheth is often regarded as the youngest son, though some traditions regard him as the eldest. They are listed in the order "Shem, Ham, and Japheth" in Genesis 5:32 and 9:18, but treated in the reverse order in chapter 10.Genesis 10:21 refers to relative ages of Japheth and his brother Shem, but with sufficient ambiguity to have given rise to different translations. The verse is translated in the KJV as follows, "Unto Shem also, the father of all the children of Eber, the brother of Japheth the elder, even to him were children born". However, the Revised Standard Version reads, "To Shem also, the father of all the children of Eber, the elder brother of Japheth, children were born." The differing interpretations depend on whether the Hebrew word ha-gadol ("the elder") is taken as grammatically referring to Japheth, or Shem.
Genesis 5:32 states that Noah had three sons when he was five hundred years old. Genesis 11:10 records that Shem was one hundred years old when his son Arphaxad was born, two years after the Flood. If Noah was six hundred years old (Genesis 7:13), then Shem was ninety-eight years old at the Flood. Ham is further implied to be the middle son in Gen. 9:24 (which says Noah realized what his "younger son" had done to him.)
The Book of Jubilees indicates in 4:33 that Shem was born in the year of the world (after creation) 1205, Ham in 1209, and Japheth in 1211.
Place in Noah's family
Main article: Sons of Noah
For those who take the genealogies of Genesis to be historically accurate, Japheth is commonly believed to be the father of the Europeans. The link between Japheth and the Europeans stems from Genesis
10:5, which states, "By these were the isles of the Gentiles divided in
their lands." According to that book, Japheth and his two brothers formed the three major races:- Japheth is the father of the Japhetic race
- Shem is the father of the Semitic race
- Ham is the father of the Hamitic race
- ...they will be kin to us, or they will fetch it from Japhet. (II.ii 117-18)
Descendants
Main article: Japhetic
In the Bible, Japheth is ascribed seven sons: Gomer, Magog, Tiras, Javan, Meshech, Tubal, and Madai. According to Josephus (Antiquities of the Jews I.6):- "Japhet, the son of Noah, had seven sons: they inhabited so, that, beginning at the mountains Taurus and Amanus, they proceeded along Asia, as far as the river Tanais (Don), and along Europe to Cadiz; and settling themselves on the lands which they light upon, which none had inhabited before, they called the nations by their own names."
The "Book of Jasher", published in the 17th century, provides some new names for Japheth's grandchildren not seen in the Bible or any other source, and provided a much more detailed genealogy (see Japhetic).
In Islam
Japheth is not mentioned by name in the Qur'an but is referred to indirectly in the narrative of Noah (VII: 64, X: 73, XI: 40, XXIII: 27, XXVI: 119). Muslim exegesis, however, names all of Noah's sons, and these include Japheth.[2] In identifying Japheth's descendants, Muslim exegesis more-or-less agrees with the Biblical traditions.[3] He is usually regarded as the ancestor of the Gog and Magog tribes, and, at times, of the Turks and Khazars. Some traditions narrated that 36 languages of the world could be traced back to Japheth.[4]Ethnic legends
In the seventh century, Isidore of Seville published his noted history, in which he traces the origins of most of the nations of Europe back to Japheth.[5] Scholars in almost every European nation continued to repeat and improve upon Saint Isidore's assertion of descent from Noah through Japheth into the nineteenth century.[6]Georgian nationalist historians such as Ivane Javakhishvili associated Japheth's sons with certain ancient tribes, called Tubals (Tabals, Tibarenoi in Greek) and Meshechs (Meshekhs/Mosokhs, Moschoi in Greek), who they claim represent non-Indo-European and non-Semitic, possibly "Proto-Iberian" tribes of Asia Minor of the 3rd-1st millennia BC.[7]
In the Polish tradition of Sarmatism, the Sarmatians were said to be descended from Japheth, son of Noah, enabling the Polish nobility to imagine themselves able to trace their ancestry directly to Noah.[6]
In Scotland, histories tracing the Scottish people to Japheth were published as late as George Chalmers' well-received Caledonia, published in 3 volumes from 1807 to 1824.[8]
Proposed correlations with deities
In the 19th century, Biblical syncretists associated the sons of Noah with ancient pagan gods.[citation needed]Japheth has been identified by some scholars with figures from other religious systems and mythologies, including Iapetus (Japetus), the Greek Titan;[9][10][11] the Indian figures Dyaus Pitar[citation needed] and Pra-Japati[citation needed], and the Roman Iu-Pater or "Father Jove", which became Jupiter.[citation needed]
Language
The term "Japhetic" was also applied by William Jones and other early linguists to what became known as the Indo-European language group. In a different sense, it was also used by the Soviet linguist Nikolai Marr in his Japhetic theory.Literature
Japheth is a major character in the Madeleine L'Engle novel Many Waters (1986, ISBN 0 374 34796 4). He is characterized as thoughtful and intelligent, a kind-hearted young man who is on good terms with feuding family members Noah and Lamech, with the seraphim, and with visiting time travelers Sandy and Dennys Murry. Depicted in the book as Noah's younger son, Japheth is barely into adulthood, but at Noah's instigation is already married. His equally kind wife is an unusually fair-skinned woman with black hair, who may have been sired by one of the nephilim.KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA --- BY. MWL. JAPHET MASATU.
FASIHI SIMULIZI.
FASIHI SIMULIZI | |
Utanzu wa | Fasihi |
Kiingereza | Oral Literature |
Tanzu za Fasihi Simulizi | |
| |
Prev | Tamathali za Usemi |
Next | Fasihi Andishi |
VIPERA VYA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI | |
HADITHI / NGANO | |
NYIMBO |
|
TUNGO FUPI | |
MAIGIZO |
Sifa za Fasihi Simulizi
- Hupitishwa kwa njia ya mdomo
- Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika
- Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
- Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
- Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
- Aghalabu huwa na funzo fulani
Umuhimu wa Fasihi Simulizi
- Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
- Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
- Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
- Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo
- Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
- Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
- Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
- Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
- Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.
FASIHI KWA UJUMLA.
FASIHI
Katika
uga wa fasihi kuna kumbo tatu muhimu zinazoipa uhai taaluma nzima ya
fasihi. Kumbo hizo ni ushairi, riwaya na tamthiliya. Uwe ukweli ama
kinyume chake lakini jambo la muhimu kufahamu ni kuwa kila kumbo katika
fasihiutawaliwa na kanuni zake na nijambo la kiuungwana kuzifuata kanuni
au Jadi husika. Kanuni hizo hutoa muongozo katika utungaji wa kazi za
kifasihi na uhakiki wa kazi hizo. Aghalabu kuzitumia kanuni huwa ni
jambo la Kiuugwana na la kheri, lakini katika zama tulizonazo sasa sio
dhambi kubwa ya kiuandishi ahesabiwayo mwandishi na wanamapokeo
anapokiuka jadi husika katika kumbo mojawapo ya fasihi andishi.
Tunapozungumzia
kanuni ama Jadi ya kiutunzi katika uga wa fasihi tunamaana ya mambo
yajitokezayo na kurudiwarudiwa mara kwa mara katika kumbo fulani ya
fasihi, kwa mfano, mambo yajitokezayo mara kwa mara katika kumbo ya
tamthiliya ni utumizi wa jukwaa, hadhira, wahusika, mtiririko wa
vitendo, dhamira na nyimbo. Kama wasemavyo waswahili “Kawaida ni kama
Sheria”, ndivyo hivyo mambo hayayanayojirudia katika kila kazi ya
kitamthiliya ndiyo yajengayo kanuni ama sheria za utungaji wa
tamthiliya.
Hapo
mwanzo kabla ya kuibuka kwa fasihi ya Kiswahili ya majaribio, kanuni
zote za ujenzi wa tamthiliya ya Kiswahili zilikopwa kutoka katika
tamthiliya ya Ulaya. Vyanzo vingi vya taarifa vinaeleza kuwa kanuni hizi
za ujenzi wa tamthiliya ziliwekwa na wanataaluma wa kimagharibi lakini
ukweli ni kwamba chimbuko la tamthiliya katika nchi na tamaduni
mbalimbali hushabihiana kwa kiasi kikubwa kwa vile uhusishwa na visakale
na matendo ya kidini. Kwa mfano, yasemekana kuwa huko Ulaya tamthiliya
ilitokana na miviga na viviga, hasa ya kidini, katika jamii ya kale ya
Wayunani, (Holman 1972, katika Mulokozi1996). Miviga hiyo iliambatana na
duru za kuzaliwa, kukua, kufa, kuoza na kuzaliwa upya ambazo hasa
zilihusishwa na Mungu aliyeitwa Dionizi, aliyeaminiwa kuwa aliuawa,
akakatwakatwa vipandevipande na baadaye akafufuka tena (Mulokozi 1996).
Pia hapa Afrika, kumbukumbu za kwanza za maigizo ya kitamthiliya
tunazipata Misri, ambako michezo ya miviga ilihusu kufa na kufufuka kwa
Mungu wa Wamisri aliyeitwa Osiris ilikuwa ikiigizwa kila mwaka kwa miaka
2000 kuanzia kama mwaka 2500KM, (Mulokozi 1996). Hii inaonyesha kuwa
chimbuko la tamthiliya katika jamii nyingi duniani linashabihiana kwa
kiasi kikubwa.
Kanuni
zilizowekwa juu ya ujenzi wa tamthiliya zilitokana na mambo
yaliyopelekeachimbuko la tamthiliya. Inaonekana wazi kuwa kanuni hizi
zilihusika na zinaendelea kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kujenga
muktadha, fani na vitendo vitendekavyo katika matambiko na mikusanyiko
ya kidini, kanuni hizo kama vile utumizi wa jukwaa, hadhira, wahusika,
vitendo, dhamira na nyimbo zinahusika moja kwa moja katika matendo
yatendekayo katika matambiko, miviga na dini za kijadi na zile za
kigeni.
Kanuni
huwa hazibakii hivyohivyo, hubadilika kufuatana na mahitaji ya jamii
kwa wakati fulani. Hapo mwanzo kanuni za Ki-Aristotle zilitumika vizuri
na kwa usahihi katika utanzu wa tamthiliya ya kiswahili. Kadri siku
zilivyoenda mbele watunzi wa tamthiliya ya Kiswahili walilazimika
kukiuka baadhi ya kanuni hizo kwa kuingiza vipengele vya fasihi simulizi
katika tamthiliya ya kiswahili ili kuifanya tasnia ya tamthiliya
andishi ifungamane na uhalisi wa kiafrika. Waandishi wengi wa tamthiliya
tulionao sasa ni wafuasi wazuri wa kukiuka kaida za Ki-Aristotle, ndipo
sasa tunaona umuhimu mkubwa wa utafii huu. Vile vile ikumbukwe kuwa
uandishi huu wa “Kimajiribio”au
ukiukwaji huu wa kaida za kiuandishi umejitokeza katika kumbo zote za
fasihi andishi, lakini utafiti huu umeshughulikia kumbo ya tamthiliyatu.
Ukiukwaji
wa kaida za Ki-Aristotle na kuingizwa kwa kanuni za U-jadi (wataalamu
wengine wanazitambulisha kanuni za U-Jadi kama fasihi ya kiswahili ya
majaribio), katika uandishi wa tamthiliyaya Kiswahili umeibua maswali
mengi kwa wadau wa fasihi.
F.E.M.KSenkoro(2011:62)
anajadili baadhi ya maswali hayo, hapa anasema “Swali ambalo hatimaye
linajadiliwa ni; je, majaribio haya yanafuata kanuni zipi? Upya una
nafasi gani katika majaribio? Na, Je, majaribio mahsusi ya fasihi fulani
yanaanza na kuisha wakati gani?
Senkorohajatoa
ufafanuzi wakutosha juu ya maswali haya. Mambo mengi ameyaacha hewani.
Utafiti huu umeibuka na majibu kwa baadhi ya maswali na kuyaacha mambo
mengine kama mada za utafiti kwa watafiti tarajali.
Kuna
tafiti kadhaa zilizofanywa na kuhifadhiwa zinazohusu tamthiliya ya
Kiswahili, tafiti nyingi kati ya hizi zinahusu uchambuzi wa vipengele
vya fani na maudhui ndani ya tamthiliya teule. Hata hivyo kwa upeo wa
ufahamu wa mtafiti hakuna mtafiti aliyewahi kujishughulisha kuhusu
mabadiliko ya uandishi wa tamthiliya ya Kiswahili kutoka U-Aristotle
kwenda U-Jadi wa Kiafrika. Wapo watafiti ambao wamefanya utafiti kuhusu
tamthiliya kwa kuchambua vipengele mahususi,baadhi ya watafiti hao ni
Omary (2011), alichunguza suala la Ukimwi lilivyo jadiliwa katika
tamthiliya za Kiswahili, Murusuri (2011), alitazama Utamthiliya katika
Ngonjera, data mahsusi alizitoka ndani ya vitabu vya Ngojera za Ukuta,
Ngojera hizi zimetungwa na mwasisi wa chama cha UKUTA na mshairi
mashuhuri Mathius Mnyampala. Vielevile, Madembwe (2011), alifanya
utafiti juu ya nafasi ya kejeli na dhihaka katika tamthiliya za Penina
Muhando. Kwa upeo wa ufahamu wa mtafiti wa utafiti huu ni kwamba hakuna
mtafiti aliyewahi kuchunguza juu ya mabadiliko ya kiuandishi
yaliyojitokeza katika tamthiliya ya Kiswahili kutoka uandishi unaofuata
kanuni za Ki-Aristotle kwenda katika uandishi wenye kuzingatia vipengele
vya Jadi ya Ki-Afrika. Kwa upeo wa mtafiti wa utafiti huu, mtafiti
mmoja tu ndiye aliyejaribu kujadili baadhi ya matendo ya kiafrika ndani
ya tamthiliya ya Kiswahili. Mtafiti Nicholaus, A, alichunguza jinsi
falsafa ya Ubuntu inavyo jadiliwa katika tamthiliya ya Kiswahili.
Nicholaus
(2011), aliteuwa tamthiliya za Penina Muhando na kuchunguza jinsi
falsafa ya Ubuntu ilivyosawiri katika tamthiliya hizo. Malengo yake ya
kufanya utafiti yalikuwa ni pamoja na kuelezea mbinu alizozitumia
mwandishi Penina Muhando katika kueleza masuala ya waafrika ikiwemo na
falsafa yao.
Katika kutekeleza lengo hilo mtafiti alitumia tamthiliya tatu za Mama Muhando, tamthiliya hizo ni Hatia, Heshima Yangu naTambueni Haki Zetu. Matokeo
ya utafiti huu yanaonyesha kuwa falsafa ya Ubuntu imejitokea kwa kiasi
kikubwa katika tamthiliya za Penina Muhando. Masuala ya waafrika
yamewasilishwa kwa njia mbalimbali kama vile Ngoma, kicheko, kilio,
kiapo, mizimu na kwa kupitia njia ya uundaji wa chama cha ZETU, kwa
kutumia njia hizi mtafiti anayataja mambo ya waafrika yaliyojitokeza
zaidi ndani ya tamthiliya teule kuwa ni pamoja na ndoa za kiafrika,
burudani, hekima, upendo, heshima, ushirikiano na kadhalika.
Pamoja
na mtafiti kufanikiwa kuonesha mambo kadhaa yanayowahusu waafrika ndani
yatamthiliya teule lakini hakuweza kuyaelezea mabadiliko ya kiuandishi
katika tamthiliya ya Kiswahili. Hakutuonesha sababu zilizopeleke
waandishi wengi wa tamthiliya ya Kiswahili kukiuka kaida za uandishi wa
Ki-Aristotle na kuzama katika Ujadi wa Ki-Afrika, hivyo kulikuwa na haja
ya kufanya utafiti
kama huu unaohusu mabadiliko ya uandishi wa tamthiliya ya Kiswahili ili
kupata data na taarifa sahihi na za kutosha ili zitumike katika uwanja
wa fasihi andishi.
Mbali
na hayo, Nicholaus alifanya Utafiti wake kwa kuchambua kazi za
mwandishi mmoja wa tamthiliya ambaye ni Penina Muhando. Utafiti huu
uliona ni vema kuchambua kazi za waandishi wawili ambao kwa hakika
wanamchango mkubwa katika kustawi kwa tasnia ya tamthiliya andishi ya
Kiswahili. Utafiti huu umechambua kazi za Ebrahim Hussein na Penina
Muhando jambo lililomwezesha mtafiti kuongeza mawanda ya kiuchambuzi na
ukusanyaji wa data katika kukamilisha utafiti huu. Pia uteuzi wa vitabu
vilivyo chambuliwa na kupelekea upatikanaji wa data za msingi, ni
tofauti na uteuzi uliofanywa na watafiti wengine kwakuwa utafiti huu
umezingatia vipindi viwili muhimu katika uandishi wa tamthiliya, kipindi
cha utawala wa kanuni za Ki-Aristotle na kipindi cha pili ni hiki
tulichonacho sasa (kipindi cha fasihi ya Kiswahili ya kimajaribio).
Subscribe to:
Posts (Atom)