Showing posts with label RIWAYA & TAMTHILIYA--KIDATO CHA 3 & 4. Show all posts
Showing posts with label RIWAYA & TAMTHILIYA--KIDATO CHA 3 & 4. Show all posts

Monday, September 9, 2019

MBINU ZA KUJIBU MASWALI : UCHAMBUZI NA UHAKIKI :USHAIRI, RIWAYA / HADITHI NA TAMTILIYA-----KIDATO CHA 3 & 4

Wanafunzi na watahiniwa wanapopata swali katika mitihani wanajukumu kubwa la kulielewa kablaya kulijibu.

Endapo mtahiniwa atakuwa anajibu swali lolote bila kulielewa matokeo yake ni hasara; atashindwa mitihani! Kushindwa si lengo la mtahiniwa yeyote yule. Ili kukwepa hilo, mtahiniwa lazima awe makini.
Mara nyingi maswali yanayoulizwa kwa watahiniwa ni yale yanayozingatia mkondo maalum. Mtahiniwa anaweza kuambiwa aanzishe, abainishe, ajadili, aeleze, alinganishe, ajadili, aeleze, alinganishe, afafanue, aonyeshe, atofautishe na kadhalika. Tunadokeza mbinu kadhaa ambazo ni za msingi katika kujibu maswali ya mtihani. 

· Maswali ya Kujadili
Kujadili ni kuhoji, kuuliza au kusaili. Suala la kujadili linahusu pande mbili. Kwa nini jambo limetokea? Kwa kawaida hutolewa kauli fulani ambayo mwanafunzi anatakiwa akubali au akatae; au yote kwa pamoja. Ni muhimu kuelewa yafuatayo:
· Swali linataka nini hasa?
· Je, kuna mambo chanya?
· Je, kuna mambo hasi? Yepi ambayo yanatakiwa kutajwa?

· Maswali ya Kulinganisha
Kulinganisha kunahitaji mambo makuu mawili. Mambo haya ni
(a) Yale yanayoeleza kufanana kwa vipengele vilivyo katika vitu tofauti na
(b) Kutofautiana kwa mambo katika vitu hivyo viwili. Baada ya kulinganisha kama swali linavyotaka, hatua nyingine muhimu ni kuangalia ufanisi wa kazi zote/vitu vyote viwili.

Maswali yanatakiwa yajibiwe kwa kufuata mtindo wa insha. Kila kipengele kinachojadiliwa kinatakiwa kihusishwe katika vitabu vyote ambavyo  vinahusishwa katika   swali.