Friday, October 3, 2014

JOKA LA MDIMU A.J. Safari{ H.P}---KIDATO CHA 3 NA 4

                                         UHAKIKI---RIWAYA

                                      JOKA    LA    MDIMU
MWANDISHI:  ABDALA  .J.   SAFARI{H.P.}
MCHAPISHAJI: HUDA  PUBLISHERS.
MWKA: 2007.


UTANGULIZI
RIWAYA    YA   JOKA  LA   MDIMU  ni   riwaya  ambayo   inaakisi  vizuri   matatizo    ya   KIUCHUMI  ya  miaka   ya   themanini  nchini  TANZANIA.  RIWAYA   hii  inaakisi   tu ,  haihakiki ,  hali  ya   maisha  katika  kipindi  cha  dhiki   ya ukosefu  wa   bidhaa   muhimu  kama   vile   nguo,  chakula ,  mafuta ,  spea  za   mashine  n.k. Wakati  huu  wa   dhiki  watu   wengine   wanateseka    na   kuumia ,  kuna   wengine    wachache   wanaotumia   nafasi   zao   kuchuma  kadri   wanavyoweza ,  hasa  kwa  njia  haramu.



UHAKIKI   WA   MAUDHUI


DHAMIRA   KUU:  Hali  ngumu   ya   Maisha.

DHAMIRA   NYINGINEZO
{1}.Rushwa   katika   jamii.
{2}.Urasimu.
{3}.Kutowajibika.
{4}.Nafasi  ya  Mwanamke katika  jamii.
{5}.Mapenzi   na Ndoa.
{6}. Uhujumu  Uchumi  na   Magendo.
{7}. Ufisadi.

WAHUSIKA

{1}. AMANI---Huyu  ni   mhusika  mkuu. Ni  dereva   taksi.  Ni  kijana  mchapa  kazi.  Ana   huruma. Ana  hekima  na   busara.Anafaa  kuigwa  na   jamii.

{2}. GRAY  KWACHA---Huyu  ni   mhusika  msaidizi. Ni  mkurugenzi   wa   Idara   ya   Fedha   za   Kigeni. Ni   malaya. Si  mtu  adilifu.  Ni  fisadi.  Anapenda  rushwa.Anafanya   biashara  za   magendo. Hafai   kuigwa.

{3}. TINO---Huyu  ni   mhusika  mkuu   msaidizi.  Ni   mvuta  kwama. Ni  baba   wa   watoto  watatu.  Ni  jasiri. Ni  mchapa   kazi.  Mwanamichezo.  Anafaa  kuigwa.

WAHUSIKA   WENGINE:

----JINJA   MALONI , DAKTARI  MIKWALA ,SHIRAZ   BHANJ ,  ZITTO ,CHECHE ,

WATOTO WA MAMA N" TILIE -------- E. Mbogo H .P} ---KIDATO CHA 3 NA 4

                                      UHAKIKI :  RIWAYA
            WATOTO  WA  MAMA  N"TILIE

MWANDISHI:   EMMANUEL    MBOGO
WACHAPISHAJI : HEKO   PUBLISHERS
MWAKA :  2002.

UTANGULIZI
 
WATOTO  WA  MAMA  NTILIE  ni  riwaya    iliyotungwa   na   mwandishi   maarufu  wa   RIWAYA   na  TAMTHILIYA  EMMANUEL   MBOGO  na   kuchapishwa  na   HEKO   PUBLISHERS  LTD   MWAKA  2002. Ni  RIWAYA  inayochambua   kwa   kina   adha   wazipatazo   akina   mama  ntilie.  Hawa  wametapakaa  mijini   huku   wakifanya   BIASHARA    YA   KUUZA  VYAKULA  ili   kutafuta  chochote  cha   kuwawezesha   kutunza   familia   zao. 
  MWANDISHI   anatueleza  kuwa  akina  mama  hawa   wanaisi   maisha    magumu . WATOTO  wao  ambao   wangewasaidia   hapo   mbeleni  hawapati   ELIMU   kutokana  na   kukosa  mahitaji   muhimu   ya    shule ,  matokeo  yake   wanajiingiza   katika  matendo   MAOVU   ikiwa  ni  pamoja   na   matumizi  ya  MADAWA  YA  KULEVYA ,UVUTAJI  BANGI  na   UJAMBAZI.


MAUDHUI
DHAMIRA
{1}.Umaskini.
{2}.Suala  la Elimu.
{3}.Suala  la  Malezi
{4}.Nafasi  ya   mwanamke   katika  jamii.
{5}. Wizi , Ujambazi  na   biashara  ya   madawa   ya   kulevya.
{6}. Mapenzi.
{7}.  Migogoro.


WAHUSIKA    WAKUU
{1}.  MAMANTILIE{ MAMA  ZITA}---Huyu  ni  mke  wa   mzee   Lomolomo. Ni  mama   mzazi  wa   Zita  na  Peter. Anajihusisha   na   biashara  ya  kuuza  chakula  gengeni.
{2}. MZEE  LOMOLOMO ---Mumewe  Mamantilie   na   baba  yao   ZITA  na  PETER.
{3}.PETER ---Ni   mtoto  wa   kiume   wa   Mamantilie   na  mzee  Lomolomo.
{4}.ZITA ---Ni   mtoto  mwingine   wa   Mzee  Lomolomo.
{5} MWALIMU   CHIKOYA.
{6}.DOTO    NA  KURWA
{7}.ZENABU.
{8}. MUSA.

TAKADINI Na Benson Hanson {MBS}----KIDATO CHA 3 NA 4



                                       UHAKIKI : RIWAYA

                                                         TAKADINI

MWANDISHI
: BENSON HANSON.
WACHAPISHAJI : METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS.


MANDHARI : RIWAYA   hii  imetumia  mandhari  ya   Vijijini  katika  nchi   ya   Zimbabwe  katika  karne  ya   19. Katika  masimulizi  haya  ya   riwaya    mandhari   yake   inaweza   kugusa   vijiji  vya  nchi  nyingi   za   KIAFRIKA  ambazo  zipo  katika   dunia   ya  tatu. {  nchi  zinazoendelea }.

 MWAKA:  2004.


 MAUDHUI

DHAMIRA KUU :


UKOMBOZI WA KIUTAMADUNI
--Ndoa.
--Mirathi.
--Uhai
--Maamuzi.
--Mgawanyo wa kazi.
--Mgawanyo wa mapato na umilikaji wa mali.
--Elimu.
--Utu.

DHAMIRA NDOGO NDOGO
---Mapenzi.
---Ndoa.
---Imani Potofu / Dhana potofu.
---Upendo.
---Ujasiri.
---Malezi ya watoto.
----Umoja na mshikamano
---Elimu.
---Nafasi ya mwanamke katika jamii na ujinsia

WAHUSIKA
TAKADINI
---Huyu ndiye mhusika   mkuu  wa   riwaya   hii.

---Ni  mtoto  wa   kwanza  wa  Sekai.
---Ni   mlemavu{ Zeruzeru } na  ana  tatizo  la   mguu.
---Kijana   wa   Kiume.
---Ni  mchapakazi  na   mtu  anayependa  kujifunza.
---Ni   mwenye   huruma.
----Ni  mtiifu.
---Ni   jasiri
---Ni    mwanamapinduzi..
---Ni  mhanga   wa  mila  na   desturi    mbaya   zinazobagua   walemavu.
----Anafaa  kuigwa   na   jamii.

SEKAI :
---Huyu  ni  mhusika  mkuu  msaidizi.
---Ni  mke  wa   kwanza  wa   MAKWATI.
---Ni  mwanamke  mchapakazi.
---Ni   mhanga  wa   mila   na  desturi  zilizopitwa  na    wakati.
---Ni    mwanamapinduzi.
---Ni  mama   mzazi   wa   TAKADINI.
---Ni  jasiri.
---Ni  mwenye   huruma.
---Ni   mwenye   busara.
----Ni  mvumilivu.
----Ni   mnyenyekevu
----Ni    mchapakazi.
----Ni   MPOLE.
---Ni   mama   mzazi    na   mlezi   mzuri   wa   familia.
---Ni   mama   mwenye  UPENDO.
---Ni    mpishi   mzuri   wa   chakula.
---Anafaa  kuigwa   na   jamii.

MAKWATI
----Ni   mume  wa   SEKAI.
---Ni   baba   mzazi  wa  TAKADINI.  
---Ni   mume  mwenye  wake   wannne,
---Ana   UPENDO   kwa  mkewe.
----Ni   mwoga.
---Ni    mkale.
Wake   wengine   wa   MZEE   MAKWATI   ni   DARAI ,  RUMBIDZAI ,


WAHUSIKA   WENGINE
CHIVERO , MTEMI  MASASA, SHINGAI , TENDAI ,   Nhamo , Maishingai , Pindai , Ambuya  Tungai , Ambupa  Shugu ,  Pedeisai ,  Mtemi  Zvedi ,  Tupfmaneyi ,  Chengatai,  Chido ,  Ambuya  Rekai ,  Mtemi  Chinjeyari.

MASHAIRI YA CHEKA CHEKA Na Theobald Mvungi. KIDATO CHA 3 NA 4.

                                        UHAKIKI :  USHAIRI

        MASHAIRI    YA    CHEKA    CHEKA

MWANDISHI :   THEOBALD  MVUNGI.
 WACHAPISHAJI :   EP  &  D. LTD 


                                                        MAUDHUI

                                       DHAMIRA
{1}.Dhamira   ya   Ukweli.

{2}.Dhamira   ya  Siasa.
----Mfumo  wa   Siasa  ya   Chama  Kimoja.
----Demokrasia.
----Suala   la   kutetea   Haki.
----Uzembe   na   Ukasuku.
----Rushwa   na   Ulanguzi.
----Ufujaji  wa  fedha  za   Umma.

{3}. Mapenzi.

{4}. Dini.

{5}. Uhusiano  wa  kimataifa.

{6}. Maisha.