BONYEZA HAPA CHINI / CLICK HERE BELOW.

Monday, September 9, 2019

MBINU ZA KUJIBU MASWALI : UCHAMBUZI NA UHAKIKI :USHAIRI, RIWAYA / HADITHI NA TAMTILIYA-----KIDATO CHA 3 & 4

Wanafunzi na watahiniwa wanapopata swali katika mitihani wanajukumu kubwa la kulielewa kablaya kulijibu.

Endapo mtahiniwa atakuwa anajibu swali lolote bila kulielewa matokeo yake ni hasara; atashindwa mitihani! Kushindwa si lengo la mtahiniwa yeyote yule. Ili kukwepa hilo, mtahiniwa lazima awe makini.
Mara nyingi maswali yanayoulizwa kwa watahiniwa ni yale yanayozingatia mkondo maalum. Mtahiniwa anaweza kuambiwa aanzishe, abainishe, ajadili, aeleze, alinganishe, ajadili, aeleze, alinganishe, afafanue, aonyeshe, atofautishe na kadhalika. Tunadokeza mbinu kadhaa ambazo ni za msingi katika kujibu maswali ya mtihani. 

· Maswali ya Kujadili
Kujadili ni kuhoji, kuuliza au kusaili. Suala la kujadili linahusu pande mbili. Kwa nini jambo limetokea? Kwa kawaida hutolewa kauli fulani ambayo mwanafunzi anatakiwa akubali au akatae; au yote kwa pamoja. Ni muhimu kuelewa yafuatayo:
· Swali linataka nini hasa?
· Je, kuna mambo chanya?
· Je, kuna mambo hasi? Yepi ambayo yanatakiwa kutajwa?

· Maswali ya Kulinganisha
Kulinganisha kunahitaji mambo makuu mawili. Mambo haya ni
(a) Yale yanayoeleza kufanana kwa vipengele vilivyo katika vitu tofauti na
(b) Kutofautiana kwa mambo katika vitu hivyo viwili. Baada ya kulinganisha kama swali linavyotaka, hatua nyingine muhimu ni kuangalia ufanisi wa kazi zote/vitu vyote viwili.

Maswali yanatakiwa yajibiwe kwa kufuata mtindo wa insha. Kila kipengele kinachojadiliwa kinatakiwa kihusishwe katika vitabu vyote ambavyo  vinahusishwa katika   swali.

KUHUSU SHAABAN ROBERT / ABOUT SHAABAN ROBERT

Shaaban Robert is to the Swahili language what Shakespeare was to English. Acclaimed as the national poet, his publications have always been the touchstone of beauty of language, purity of spirit, and deep wisdom informed by African and Swahili culture in particular, but imbued with respect for and understanding of other cultures. Most prominent of his work is Kusadikika (To be believed), an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. Published at the height of colonial occupation in Tanzania.

Shaaban Robert kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza. Akikubalika kama mshairi wa taifa, vitabu vyake daima vimekuwa kipimo cha juu cha uhondo wa lugha, usafi wa nia na hekima kutokana na utamaduni hususan wa Kiafrika na Waswahili lakini pia kwa jnsi alivyoelewa na kusheshimu tamadui nyingine. Katika vitabu vyake Kusadikika ndicho maarufu kushinda vyote. Hii ni hadithi ya kiistara juu ya nchi ambako dhuluma inatawala kinyume na haki, sheria na utu. Kitabu kilichapishwa wakati ukoloni umetanda nchini Tanzania.

WASIFU WA SITI BINTI SAAD-----RIWAYA / HADITHI-----BY SHAABAN ROBERT

Siti binti Saad alikuwa mwanamke wa kwanza Zanzibar kusimama jukwaani na kuimba nyimbo za taarab. Katika kitabu hiki, Shaaban Robert anaelezea juu ya maisha ya umaskini na hali ya chini aliyoishi msanii huyu, katika jamii ya Zanzibar iliyokitwa na tabaka za kijamii miaka ya kwanza ya karne ya ishirini. Licha ya kuwa sura yake ati haikuwa nzuri, alifikia hali ya juu ya nyota wa uimbaji wa taarabu akapendwa na wapenda taarabu si Zanzibar tu na Afrika ya Mashariki, lakini pia alipendwa hadi Misri na India. Kwa wapenzi wa taarab bado ni malkia, sawa na alivyokuwa Om Kulthum wa Misri. 
 Siti binti Saad was the first woman Taarab singer in Zanzibar. In this book Shaaban Robert looks at the background of the singer: poverty and low birth, in a society riven by class and race in early 20th century Zanzibar. Despite her so-called bad looks, she became a star whose voice was recognised and loved by many, not only in Zanzibar and East Africa, but as far as Egypt and India. She was and remains to taarab lovers, the equivalent of Egypt’s Om Kulthoum.

Saturday, September 7, 2019

SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU

Habari natangazia, Kuwapatia uhondo
Nchini Tanzania,   Kijiji cha  Loliondo
Watu viguu na njia, Wanoenda kwa vishindo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Siku imepambazuka, Naamshwa kwa kelele
Najifunga yangu shuka, Kutazama walo mbele
Tayari washazunguka, Kwa Kasisi Ambakile
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Miujiza imefika,  Babu yeye keshaota
Wote mloathirika, Anzeni kujikokota
Loliondo mkifika,  Mizizi inatokota
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Iwapo una nafasi,  Usiende mhimbili
Ondoa na wasiwasi, Loliondo kuna dili
Dawa bei ni rahisi, Kikombe ni buku mbili
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kashinda madakitari, Walosoma hadi ng’ambo
Magonjwa yote hatari, Yalokuwepo kitambo
Eti mpaka kisukari,  kweli babu ana mambo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Ukimwi unatutisha, Ugonjwa kama adhabu
Waganga wamechemsha, Kutafuta matibabu
Kama mbinu zimekwisha, Kajaribuni kwa babu
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kwa babu kuna vioja, Kabla kutoa tiba
Hutangaza yake hoja, Dawa msije kuiba
Mnapata mara moja, Sio kunywa mkashiba
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Wala msifanye pupa,  Walokwenda ni umati
Babu dawa akikupa,  Kunywa  kwa kombe la bati
Usipeleke na chupa, Ukayavunja  masharti
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Aponya kila madhara, Hili wengi wanakiri
Pengine ni  biashara, Katumia muhubiri
Kujitoa  ufukara,  Ajipe na utajiri
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Mara bibi wa tabora, keshaibuka na yake
Kujiona ndio bora, Na yeye afaidike
Watu kweli ni wakora, Jamani tuwajibike
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Sijui kama ya kweli, Msije mkasusia
Mi nahisi utapeli,  Mbuzi ndani ya gunia
Dawa sijaikubali,   Maajabu ya dunia?
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Namefika kaditama,  Dawa zinanitatiza
Babu ataniandama,  Malenga kuniapiza
Ninaogopa lawama,  Shairi nimemaliza
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
HAMZA A. MOHAMMED